UKURASA WA 723; Kama Unachagua Mwenyewe, Kwa Nini Uchague Hovyo?

By | December 23, 2016

Kwa mfano nikakupa cheki ya benki ambayo tayari imeshawekwa sahihi na kuandikwa jina lako kwamba wewe ndiye mlipwaji, lakini ile sehemu ya kiasi gani ulipwe nikakuachia ujaze mwenyewe. Na nikakuonesha kwamba salio kwenye akaunti hiyo unayoenda kutoa fedha ni bilioni tano. Utaandika kiasi gani kwenye cheki hiyo na uende kuchukua? Na hapa hakuna lolote unalodaiwa, ni malipo ya uvumilivu wako mkubwa kwenye kitu ulichokuwa unafanya. Je utaandika laki moja? Au milioni moja? Au milioni kumi, hamsini au mia?

Hivi ndivyo asili inavyotupa utajiri kwenye maisha yetu. Tunapewa cheki ambayo imeshawekwa sahihi, kazi yetu ni kuandika kiwango halafu tunakipata. Yaani hakuna wa kutupangia tuandike kiwango gani kwenye cheki hiyo. Lakini cha kushangaza, watu wanaandika kiasi kidogo mno kwenye cheki hii, halafu kila siku utawaona wakilalamika kwamba maisha ni magumu.

Kuna kitu kimoja ambacho ni msingi wa utajiri wote na maisha ya mafanikio. Uzuri wa kitu hiki ni kwamba tuna nguvu ya kuchagua sisi wenyewe tunatakaje na tunataka kwa kiasi gani. Hakuna wa kutuingilia kwenye uchaguzi wetu.

Kitu ninachozungumzia hapa ni tabia.

Hivi unajua tabia yako ina mchango mkubwa sana wa hapo ulipo?

Tabia yako imeathiri biashara zako, imeathiri kazi zako na hata maisha yako kwa ujumla. Lakini unachopaswa kujua ni kwamba, hakuna aliyekulazimisha uwe na tabia ambazo unazo sasa. Ulichagua wewe mwenyewe na unaendelea kuzilea wewe mwenyewe.

Wema au ubaya, uchapakazi au uvivu, umakini au uzembe, shukrani au lawama zote ni tabia ambazo unachagua wewe. Hakuna anayekulazimisha, ni wewe mwenyewe unakubali kuishi na tabia ulizochagua.

Hivyo basi, hebu mulika tabia zako zote kwenye maisha yako ya kawaida, maisha ya kazi na ya biashara, angalia ni tabia zipi zinakurudisha nyuma. Achana na tabia hizo na jijengee zile tabia zenye manufaa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.