UKURASA WA 749; Maswali Matatu Muhimu Kujiuliza Kabla Ya Kuchukua “RISK”…

By | January 18, 2017

Utakuwa umesikia mara nyingi sana kwamba watu waliofanikiwa ni watu wanaochukua risk, kwa kiingereza wanawaita RISK TAKERS. Lakini ambalo huwezi kusikia ni kwamba karibu kila mtu anachukua risk, ila wanaofanikiwa wanachukua risk zinazowanufaisha wakati wasiofanikiwa wanachukua kila risk na hivyo kujikuta wanazidi kurudi nyuma.

Kuchukua risk maana yake ni kufanya jambo ambalo ni la hatari. Ni kufanya jambo ambalo huna uhakika kama litakwenda vizuri kama ulivyotarajia. Ni kufanya jambo ambalo hujawahi kufanya tena na wakati mwingine hakuna mwingine ambaye ameshalifanya.

Bilionea mwekezaji, Warren Buffet anasema kwamba zipo sheria mbili kuu za uwekezaji, sheria ya kwanza kamwe usipoteze fedha, na sheria ya pili ni kuhakikisha unafuata sheria ya kwanza. Kwa Warren hii ni njia nyingine ya kusema kwamba unahitaji kuchukua risk ambazo hazitakuangusha.

Je wewe unawezaje kuchukua risk zenye faida au zisizoumiza kama wanavyochukua watu waliofanikiwa?

SOMA; Hatua Za Kuchukua Kama Huwezi Kudhibiti Hasira Zako…

Jibu ni kwamba yapo maswali matatu muhimu ya kujiuliza kabla ya kuchukua risk yoyote kwenye maisha yako, kazi au biashara zako.

Swali la kwanza ni je ipi faida ninayoipata kwa risk hii ninayotaka kuchukua.

Lazima uanze kuangalia unanufaikaje na kile ambacho unakwenda kufanya, kama mambo yatakwenda kama ulivyopanga. Kwa kujua unanufaikaje kutakufanya ujue njia sahihi ya kufuata.

Swali la pili ni kama mambo yatakwenda tofauti na unavyotarajia, utaumia kiasi gani?

Kwa lugha nyingine ni hasara ipi utakayoipata kama mambo hayatakwenda kama ulivyopanga? Hapa unahitaji kujua kabisa unaweza kutumbukia kwenye shimo gani.

Swali la tatu; je naweza kuishi na ile hasara nitakayoipata? Huu ni mwendelezo wa swali la pili, ukishajua itakuwaje pale mambo yanapokuja tofauti na matarajio yako, unahitaji kujua kama unaweza kuishi na matokeo hayo. Je unaweza kuishi na matokeo ambayo hukutegemea kufanya?

Kwa kujua maswali hayo mawili ya kwanza, na kuwa tayari kwa swali la tatu, unaweza kuchukua hatua. Lakini kama hasara utakayoipata huwezi kuishi nayo, yaani itapelekea maisha yako kuwa hovyo zaidi, ni vyema usichukue risk hiyo kwa sasa.

Chukua ile risk ambayo hata kama utapoteza, basi maisha yako hayatasimama, mambo yataendelea kwenda kama kawaida.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

One thought on “UKURASA WA 749; Maswali Matatu Muhimu Kujiuliza Kabla Ya Kuchukua “RISK”…

  1. Pingback: UKURASA WA 752; Ujuzi Na Mtazamo… – Kisima Cha Maarifa

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.