UKURASA WA 812; Jinsi Ya Kuwakaanga Watu Kwa Maneno Yao Wenyewe….

By | March 22, 2017

Hata kama hutawakosea watu kitu chochote, hata kama utakazana kufanya yako, kupambana ili kutimiza ndoto zako, wapo watu ambao watajitolea kukuchukia. Kwa ile dhana tu kwamba wewe kuna makubwa unafanya, ambayo yamewashindwa wao, inatosha kutengeneza wivu na hatimaye kuleta chifu.

IMG-20170306-WA0003

Hivyo wakati wewe unakazana kufanya yako, wapo watu watakaokua wanakuongelea vibaya. Watakuja na hadithi zao kuhusu wewe, jinsi ulivyo na roho mbaya, jinsi usivyojali na kadhalika, vitu ambavyo unajua kabisa hufanyi.

Kwa hali ya kawaida ya binadamu, utapenda na wewe kuongea mabaya ya watu hao, au kubishana nao kwa mabaya yao. Lakini hilo halitakusaidia wewe (litakupotezea muda) na pia halitawasaidia wao (litawafanya watafute njia za kudhibitisha wanachosema).

Hivyo, ili kuepuka hayo yote, na kama unataka kuwakomesha kweli wale wenye wivu na chuki wanaozusha maneno, wewe aongelee vizuri. Wakati wao wanasema maneno mabaya juu yako, wewe sema maneno mazuri juu yao. Hilo litawavuruga na kuwaumiza sana. Hawataweza kuendelea kusema mabaya juu yako, na kadiri unavyozidi kufanikiwa, inazidi kuwaumiza zaidi, na wakati huo hawana cha kufanya.

SOMA; Maneno Ya Kujifariji Yanayowafanya Watu Kuendelea Kuwa Masikini, Yaepuke.

Hii ni njia ambayo haitakupotezea wewe muda wako na haitawapa kichocheo cha kuendelea kuongea mabaya yao. Maana unaposhindana nao kwa kuwaongelea mabaya, unakuwa umeweka mafuta ya taa kwenye moto, unauchochea zaidi.

Muhimu; kama anayekusema kwa mabaya ni mpumbavu, unahitaji kuwa makini zaidi, maana wapumbavu huwa hawajifunzi, na wewe kuwasema kwa mazuri, wanaweza kutumia njia hiyo kukusema kwa mabaya zaidi. Hivyo njia pekee ya kupambana na mpumbavu, ni kuachana naye haraka sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

2 thoughts on “UKURASA WA 812; Jinsi Ya Kuwakaanga Watu Kwa Maneno Yao Wenyewe….

  1. Mary Materu-Behitsa

    Njia ya kupambana na mpumbavu ni kuachana naye haraka sana. Swali: Nitamtambuaje mpumbavu?

    1. Makirita Amani Post author

      Utamtambua mpumbavu kwa tabia zake, ambazo lazima azioneshe wazi kabisa.
      Tabia moja kuu ya mpumbavu ni kutokujua kitu na kutokutaka kujua au kujifunza hicho ambacho hajui.
      Yaani anakuwa hajui, halafu anaamini yeye ndiye anayejua, zaidi yake.
      Ukishakutana na mtu wa aina hiyo, kimbia kwa sababu kikubwa atakachokuletea ni matatizo.

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.