UKURASA WA 739; Uhuru Pia Unatokana Na Uvumilivu Wa Wengine…

By | January 8, 2017

Ni kawaida kwetu binadamu kuona kwamba kile tunachoamini sisi ndiyo sahihi, na wale ambao wanaamini tofauti na tunavyoamini sisi wanakosea. Kwa hali hii kuna watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kuwapinga wengine badala ya kutumia muda huo kuhakikisha wanakuwa bora zaidi.

Watu wote hawawezi kuamini kitu kimoja, au kukubaliana kwenye kila kitu. Kila mtu anayo haki ya kuamini vyovyote anavyotaka kuamini.

SOMA; Maana Halisi Ya Uhuru Wa Kweli Kwenye Mafanikio…

Hivyo uhuru wetu wa kweli, sisi kama wana mafanikio ni kuweza kuwakubali watu vile walivyo, kuwaheshimu kwa kile wanachoamini na kuona tunawezaje kushirikiana kwa yale tunayoweza kuwa pamoja. Wakati mwingine tunahitaji kuvumilia wanachoamini wengine hata kama kinapingana kabisa na kile tunachoamini sisi, hasa inapohusisha maeneo yanayoshika hisia zetu kama dini na siasa.

Mara nyingi unahitaji kuacha au kuwa tayari kupoteza kile ambacho ungepeswa kupata kwa manufaa ya jamii kwa ujumla. Lazima tuwe tayari kukubali kwamba baadhi ya mambo yatakwenda tofauti na namna tulivyotarajia. Kwa njia hii tutaweza kushirikiana na kila mtu na kuweza kufanya makubwa.

SOMA; Uhuru Chanya Na Uhuru Hasi…

Wewe kama mwana mafanikio usije kamwe ukabagua ni mtu gani unaweza kushirikiana naye na yupi huwezi, hasa kwa kigezo cha imani tofauti au uwezo tofauti. Pia usije kubagua kwa nani ujifunze kutokana na tofauti ya imani. Hata mtu ambaye anapingana na wewe kwenye kila kitu, bado kuna namna mnaweza kushirikiana na pia kujifunza kutoka kwake.

Kuwa mvumilivu na kuwa tayari kupoteza wakati mwingine, ili kuandaa mazingira ya kufanikiwa ziadi baadaye.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.