Watu wengi wamekuwa wakijidanganya sana mwanzoni mwa biashara. Wamekuwa wakidhani kuna vitu vingi wanahitaji kufanya ili biashara zao ziweze kuanza vizuri. Hivyo watu huhangaika na vitu vidogo vidogo ambavyo ukiviangalia kwa undani, havina uhusiano wa moja kwa moja na mteja kulipa fedha.
Unapoanza biashara, mara nyingi unakuwa peke yako, na hivyo wewe mwenyewe ndiye unayefanya kila kitu kwenye biashara hiyo. Ili uweze kuipeleka biashara hiyo mbele, unahitaji kuwa mwangalifu sana na namna unavyotumia muda wako na vitu unavyovipa vipaumbele.
Hivyo badala ya kufikiria kufanya kila kitu, weka vipaumbele kwenye mambo yafuatayo;
SOMA; Usilazimishe Kila Mtu Kuwa Mteja Wako…
- Kukutana na wateja na watu wanaoweza kuwa wateja wa biashara yako, kuwaeleza umuhimu wa wao kununua kutoka kwako, licha ya kuwepo na wengi wanaouza unachouza.
- Kuomba wateja wako wa mwanzo wakupatie watu wanaofaa kuwa wateja wako na uongee nao pia.
- Kuhakikisha wateja wapya wameijua na kusikia kuhusu biashara yako na pia wamehamasika kununua.
- Kuhakikisha mteja anapata kile ambacho umemwahidi atapata.
Muda mchache ulionao, wekeza kwenye vitu ambavyo vinazalisha fedha, maana fedha ndiyo inayowezesha biashara yako kukua. Usivipe vitu vyote uzito sawa, weka vipaumbele kwenye yale mambo ambayo yanapelekea wewe kumuuzia mteja bidhaa au huduma zako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK