UKURASA WA 809; Kama Huna Muda Sasa, Hutakuwa Na Muda Baadaye…

By | March 19, 2017

Kisingizio cha sina muda kimekuwa kinatumika na watu ambao hawapo tayari kuchukua hatua kwa wakati ambao wanao. Wanaona siku zijazo watakuwa na muda mwingi zaidi wa kufanya kile wanachotaka kufanya.

IMG-20170316-WA0010

Lakini muda huwa hauendi hivyo, kama huna muda sasa, hutakuwa na muda baadaye pia. Kwa sababu hakuna muda zaidi unaopatikana, muda ni ule ule, masaa 24 kwa siku. Hivyo kusema utapata muda zaidi baadaye, ni kujidanganya tu na kujiondolea hali ya kujisuta.

Najua unachosema ni kwamba sasa hivi una mambo mengi, lakini baadaye mengi yatapungua. Ninachotaka kukutahadharisha ni kwamba mambo huwa hayapungui hata siku moja, na mbaya zaidi yamekuwa yanaongezeka kadiri siku zinavyokwenda. Kama kuna unalofanya unafikiri likiisha basi utaanza, kabla hata halijaisha utajikuta unaanza jingine.

Kama unasema kinachokuzuia sasa ni kazi, au familia, au masomo, jua tu ya kwamba chochote unachotumia kama sababu sasa, kikiisha kuna kingine kinajaza pale, hivyo kwa hakika, hutapata muda, kwa dhana yako ya kusubiri mambo yaishe.

SOMA; Jiwekee Ukomo Wa Muda…

Sasa je nini unaweza kufanya?

Unachoweza kufanya ni kimoja, weka vipaumbele vyako, jua yapi ni muhimu na jipange kwa muda ulionao sasa kuyafanya. Anza mara moja kufanya, hata kwa hatua ndogo sana kile ambacho ni muhimu kwako kufanya. Usisubiri mkapa upate muda, hutaupata kwa sababu utajikuta una vitu vingi zaidi vya kufanya.

Weka vipaumbele, fanya yale ambayo ni muhimu kwa sasa, lolote muhimu lisisubiri mpaka upate muda, muda unao sasa, ni wewe kuupangilia vizuri.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

One thought on “UKURASA WA 809; Kama Huna Muda Sasa, Hutakuwa Na Muda Baadaye…

  1. Pingback: UKURASA WA 811; Upo Muda Wa Kutoa, Lakini Haupo Wa Kurudisha… – Kisima Cha Maarifa

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.