Magonjwa yanayosababishwa na vizuri ni magonjwa ambayo huwa yana changamoto sana kwa sababu vizuri huwa wanasambaa haraka na pia ni wagumu kutibika. Hii ni kwa sababu vizuri wanaweza kuwa kama viumbe hai na wakati mwingine wakawa kama siyo viumbe hai, yaani wakawa kama jiwe tu. Dawa zinazotengenezwa kuua, zina uwezo wa kuua viumbe hai kwa sababu huenda kuingiliana na mfumo wa maisha na kuukatisha hivyo kupelekea kifo. Sasa kirusi kikijiweka kwenye hali ambayo siyo ya kiumbe hai, dawa inashindwa kufanya kazi.
Lengo langu siyo kukuambia kuhusu dawa za virusi, bali kukueleza kirusi ambacho kimekuwa kinaua ndoto za wengi. Kirusi hichi kinasambaa kwa kasi sana, na pia ni kigumu kuua.
Kirusi ninachozungumzia hapa ni hofu, hofu huwa inasambaa kwa kasi ya ajabu. Na hofu ikishaingia kwenye vyombo vya habari, ni kama moto umewekwa mafuta. Kwa kuwa zama hizi tunazoishi kila mtu ana uwezo wa kutoa habari, kupitia mitandao ya kijamii, basi hofu imezidi kuwa kirusi mkali. Kwa sababu mtu mmoja, anaweza kuwa na hofu zake, akaanza kuzisambaza na baada ya muda mfupi kila mtu ameshaambukizwa hofu.
Ubaya wa hofu pia ni ngumu kutibu kwa sababu unakuwa umeimiliki, yaani hofu inaanzia ndani yako mwenyewe, hata kama umesikia tu kwa wengine. Unajipa nafasi kwenye hofu hiyo na kuona namna mambo yatakavyokuwa hatari kwa upande wako, hilo linakufanya ushindwe kupiga hatua kabisa kwenye maisha yako.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoua Ndoto Zako Kubwa Za Mafanikio.
Kuondokana na hofu hizi zinazoua ndoto za wengi, ni sawa na kuondokana na magonjwa ya virusi, kinga ni bora kuliko tiba. Hivyo jikinge na hofu za wengine, usikubali watu wakupandikize hofu zao. Hivyo kuwa makini sana na vyombo vya habari unavyofuatilia na pia aina ya marafiki unaokuwa nao kwenye maisha ya kawaida na hata kwenye mtandao. Kaa mbali na watu ambao muda wote wanatengeneza tu hofu, hata kama mambo ni mazuri, wanaanza kutengeneza hofu kwamba baadaye yatakuwa mabaya.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK
Asante