UKURASA WA 836; Fukuza Nusu Ya Wateja Wako…

By | April 15, 2017

Mfanyabiashara yeyote akisikia anashauriwa kufukuza wateja anaweza kumwona anayemshauri kama amechanganyikiwa hivi.

IMG-20170217-WA0002

Umeanzisha biashara ili kutoa bidhaa na huduma kwa wateja, sasa kwa nini uwafukuze tena? Wakati kadiri unavyokuwa na wateja wengi ndivyo biashara yako inavyopata faida zaidi na kukua zaidi.

Ni rahisi kusema hivyo kwa nadharia, lakini turudi kwenye vitendo na uhalisia. Katika wateja ulionao, wapo ambao wanachelewa kulipa, wapo ambao ndiyo wanalalamikia kila unachofanya na wapo ambao hawaridhishwi na chochote unachofanya.

Kwa upande wa pili wapo ambao wanathamini sana kile unachofanya, wanalipa kwa wakati, wanawaambia wengine kuhusu biashara yako na wanakushauri vizuri. Je ni aina ipi kati ya hizo mbili za wateja unataka zaidi?

Bila shaka unataka aina ya pili ya wateja, wale ambao wana mchango mzuri kwenye biashara yako, na hivyo wewe kuweza kutoa mchango mzuri zaidi kwao.

Sasa ili uweze kupata hao zaidi, kwanza lazima ufukuze wale wateja wa aina ya kwanza, wale ambao wanafanya biashara yako iwe ngumu sana.

Utaniuliza kwa nini niwafukuze badala ya kwenda nao wote kwa pamoja?

Na mimi nitakujibu rasilimali unazotumia kwa wateja wasioridhishwa na unachofanya, ni kubwa sana ambazo kama ungezielekeza kwa wale wanaoridhishwa, ungenufaika zaidi. Wale wanaokusumbua wanatumia muda wako mwingi na nguvu zako nyingi kujaribu kuwaridhisha au kuwadai, wakati wapo ambao hawanyonyoi rasilimali zote hizo.

Kinachotokea sasa, ukishakuwa na wateja wasumbufu wengi, unajikuta unashindwa hata kuwahudumia wale wateja wazuri wachache, na hatimaye biashara yako kupoteza wale wateja wazuri.

Ndiyo maana nakuambia fukuza nusu ya wateja wako, wale wote ambao wanasumbua kwenye biashara, achana nao na weka nguvu zako kuwahudumia vizuri wale wanaoridhishwa na biashara yako, ili wawalete wengi zaidi wa aina yao.

Ni lazima utengeneze utofauti fulani kwenye biashara yako, ambapo mteja anaona thamani kubwa ya yeye tu kuwa mteja wako, kabla hata hajapata bidhaa au huduma unayotoa.

Usiwe na biashara na kujiambia mteja wako ni mtu yeyote, utakuwa huna mteja na wale utakaowapata watakusumbua sana.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.