UKURASA WA 842; Hatua Kubwa Kubwa…

By | April 21, 2017

Kuchukua hatua pekee haitoshi, unahitaji kuchukua hatua kubwa kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa na kuweza kufikia ndoto zako kubwa. Kwa sababu wapo watu ambao wamekuwa wanasema nimefanya kila kitu, lakini bado biashara yangu haikui, au bado kazi yangu hainilipi. Unapochunguza kwa undani, unagundua kwamba hatua wanazochukua ni ndogo sana.

IMG-20170321-WA0000

Unahitaji kuchukua hatua kubwa, zaidi ya wengine wanavyochukua, kwa sababu mtego mbaya sana ni kufanya vile ambavyo wengine pia wanafanya. Unahitaji kwenda hatua ya ziada sana kama kweli unataka kutoka hapo ulipo na kufika mbali zaidi.

Fanya kila kitu kwenye biashara yako kwa ukubwa, fikia watu wengi, toa huduma bora kabisa na wape watu zaidi wa wanachotegemea kupata.

SOMA; HIZI NDIO HATUA KUMI ZA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KWENYE MAISHA YAKO

Kwenye kazi pia, chukua hatua kubwa sana, wahi eneo lako la kazi mapema zaidi, na chelewa kuondoka, maliza majukumu yako kwa wakati na toa matokeo makubwa zaidi ya unavyotegemewa, au wanavyotoa wengine.

Katika kuchukua hatua kubwa kubwa, usiangalie sana wengine wanafanyaje au wanasemaje. Kwa sababu ukiwaangalia utaridhika haraka na kuona tayari upo mbali, hivyo utarudi nyuma na kuchukua hatua ndogo. Ukiwasikiliza wanasemaje utakata tamaa maana hawatafurahishwa na kitendo cha wewe kuchukua hatua kubwa, hivyo watakupinga na kukukatisha tamaa.

Kipaumbele chako kikuu kiwe kuchukua hatua kubwa kubwa, kwa lile jambo ambalo unajua ni muhimu kabisa. Hatua ndogo ndogo na maneno waachie wengine.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.