UKURASA WA 845; Kabla Ya Sisi Na Baada Ya Sisi…

By | April 24, 2017

Kabla ya sisi palikuwepo na maisha hapa duniani. Walikuwepo watu ambao walikuwa na matatizo na changamoto zao. Walikuwa wakikazana kuifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi. Na walikuwa wakiweka kila juhudi kuhakikisha wanapata kile walichotaka. Leo hii wengi sana hawapo nasi tena.

IMG-20170303-WA0002

Baada ya sisi watakuwepo watu pia hapa duniani, watakuwa na matatizo na changamoto zao kwa kipindi hicho. Watakuwa wakikazana kutatua matatizo yao, wataweka juhudi kuhakikisha wanapata wanachotaka. Wakati huo wengi wetu hatutakuwepo.

Hii inatukumbusha kwamba wakati pekee tulionao ni sasa, huu ndiyo wakati ambao tunaweza kufanya chochote ambacho tunataka kufanya. Wakati uliopita hatuwezi kuutumia tena, na ule unaokuja hakuna mwenye uhakika nao.

SOMA; Tofauti Ya Wengi Na Sisi Katika Utajiri…

Sasa kwa wale marafiki zangu ambao ni wataalamu wa kusema kesho, na kesho zenyewe hazijawahi kufika, wanapaswa kukumbuka hili kila mara. Unapojiambia kesho, jua huna udhibiti wa aina yoyote ile kwenye hiyo kesho. Yako ni leo, itumie au ipoteze, kesho hujui kwa hakika itakuwaje.

Na pia tukumbuke wajibu wetu mkuu ambao ni kuifanya dunia kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi, kwa kuweka juhudi kwenye kazi tunazofanya, ambazo zinaongeza thamani kwa wengine, kwa kuwatatulia matatizo yao au kuwapa mahitaji yao. Hiyo ndiyo alama pekee tunaweza kuiacha hapa, mengine yote yatapita na watakuja wengine kuendeleza yao.

Kwa muda ulionao sasa, fanya lililo sahihi, na epuka sana kuupoteza kwa mambo yasiyokuwa na tija kwako. Maisha ni mafupi, yaishi kwa ukamilifu wake.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.