Mimi siyo mnafiki lakini…… maelezo yanayofuata hapo ni ya unafiki mtupu.
Au mimi siyo mbaguzi lakini…. sentensi itakayofuata hapo ni ya kibaguzi.
Nafikiri unapata picha, kama vile, sitaki kupinga lakini…… unajua kinachofuata hapo.
Matumizi yatu ya lugha na maneno yanatuwezesha watu kutusoma wazi, na kujua kile ambacho tunaficha kusema. Na hilo halitusaidii zaidi ya kuwafanya wengine watuone sisi siyo waaminifu.
Unaposema wewe siyo mnafiki, halafu ukatoa maelezo ya kinafiki, unamtengenezea mtu picha gani? Ya kwamba wewe ni mnafiki unayejificha.
SOMA; UKURASA WA 875; Neno Linalofuata Baada Ya Lakini, Linapinga Lililotangulia Lakini…
Nimekukumbusha hili leo rafiki yangu uache kutoa maelezo yanayoipinga yenyewe na kukupunguzia unafiki.
Sema kile unachojua ni sahihi, kile unachosimamia, bila ya kutaka kufichaficha. Watu wanapojua unasimama wapi, wanakuheshimu kwenye kile unachosimamia. Lakini unapokuwa upande huu, mara upande ule, watu wanashindwa kuelewa unasimama wapi, na kukuona wewe siyo halisi.
Sema kile kinachoeleweka, na namna unaowaambia wanavyoweza kuelewa, usijipinge wewe mwenyewe.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog