UKURASA WA 880; Watu Wabaya Katikati Ya Watu Wabaya….

By | May 29, 2017

Likianza swala la nani yupo sahihi na nani anakosea, kila mtu atajiona yupo sahihi na wengine ndiyo wanaokosea, sisi ni wema na wengine ni wabaya.

Lakini ukweli ni kwamba, sisi wote ni watu wabaya tunaoishi katikati ya watu wabaya. Na pia ni watu wema tunaoishi katikati ya wema. Yote hayo ni sawa.

Hii inatukumbusha kwamba kila mmoja wetu kuna makosa anafanya, na hivyo njia pekee ya kuweza kwenda pamoja na salama hapa duniani, ni kuchukulia kwa vile tulivyo. Kila mtu ajitahidi kadiri ya uwezo wake kuwa mtu bora zaidi, lakini tusitegemee kila mtu awe kama malaika.

Kwa sababu kila kitu kimoja utakachochagua kwenye maisha yako, kuna vingine ambavyo utaviacha, na hivyo vitaweza kuwaathiri au kuwanyima mazuri wengine.

Jukumu letu ni kukazana kuwa bora, na kuwa wa msaada kwa wengine, kadiri ya uwezo wetu. Tukijifunza kwa makosa tunayofanya na kuendelea kuwa bora zaidi. Tusitegemee kufikia ukamilifu na pia tusitegemee wengine kuwa wakamilifu.

SOMA; Angusha Na Tawala Watu Hawa Wawili Ili Uweze Kuwa Na Mafanikio Makubwa.

Tuvumiliane kwa sababu kila mtu anakazana kuyaelewa haya maisha, wengine wana misingi mizuri wengine hawana misingi na hivyo kujaribu kila wanachoweza kujaribu.

Juhudi zetu binafsi na ushirikiano wetu na wale wanaotuzunguka, ndivyo zitakazotuwezesha kuwa na jamii salama na hata dunia salama. Siyo rahisi, lakini ni kitu cha kufanyia kazi na kuwa bora zaidi kila siku.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.