Kuna siku unaweza kuona wingu zito kabisa, likazuia usione jua kabisa. Lakini unafikiri jua linakuwa limeenda wapi? Jua linakuwa pale pale, hata wingu liwe zito kiasi gani, jua huwa halipotei, wingu litaziba kwa muda tu.
Na uzuri ni kwamba, wingu halikai muda mrefu, kwa sababu pale lilipo siyo asili yake, baada ya muda litaondoka na jua litaendelea kuonekana kama kawaida. Jua lipo pale lilipo na linaendelea kuwepo kwa sababu pale ndiyo asili yake. Pale ndipo jua linapaswa kuwa na lipo hapo.
SOMA; Kila Kitu Kinarudi Kwenye Asili Yake…
Hivi ndivyo maisha ya mafanikio pia yalivyo.
Mafanikio yako yanaweza kuzibwa kwa muda tu, ila hayawezi kupotezwa kabisa na kitu chochote. Matatizo na changamoto vinaweza kukuzuia kwa muda usifanikiwe, lakini haviwezi kudumu milele. Kama wewe utaendelea kufanya kile unachofanya, kwa sababu ndiyo umechagua kufanya, basi utapata kile unachotaka kupata, bila ya kujali unapitia nini kwa sasa.
Kama vile ambavyo jua haliachi kuwaka kwa sababu kuna mawingu, nawe pia usiache kufanya kwa sababu unakutana na vikwazo au changamoto. Wewe fanya, kama vile vitu hivyo havipo, na endelea kufanyia kazi ili kuvuka changamoto hizo.
Na mwisho wa siku, changamoto zitakukimbia, na utabaki na ushindi, kama ambavyo wingu hupotea na jua kubaki likiwaka vizuri.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog