UKURASA WA 898; Kutoroka Siyo Suluhisho….

By | June 16, 2017

Kuna wakati tunakutana na changamoto au matatizo ambayo yanaomekana ni makubwa kuliko uwezo wetu. Kila tukiyaangalia tunaona hakuna namna tunaweza kupambana nayo. Sasa kwa kuwa akili yetu haipendi tuteseke, inachofanya ni kutafuta njia ya kutoroka.

Na hapo tunaona mengi ya kufanya, lakini siyo kulikabili tatizo.

Tunaanza kuangalia nani kasababisha mpaka tuwe kwenye tatizo lile, tunaanza kukusanya ushahidi namna gani wengine wamechangia sisi kufika pale.

Tunaanza kutafuta mambo mengine ya kufanya ili kuondoa akili zetu kwenye tatizo. Tunaangalia tv, tunatembelea mitandao ya kijamii, tunapiga soga au kutumia vilevi.

Lakini hayo yote hakuna kinachotatua tatizo, bali tunajifurahisha tu kwa muda. Huenda kweli tutamjua aliyesababisha, lakini sasa inasaidia nini? Tatizo tayari unalo. Au unapata kilevi, unasahau kwa muda, ila kinapoisha tatizo linarudi pale pale.

Suluhisho la tatizo lolote lile ni kulitatua, kuhakikisha unapata kitu cha uhakika cha kufanya kuvuka tatizo hilo. Kujitoa na kuweka kazi kuhakikisha hukwamishwi na tatizo hilo.

SOMA; Tatizo Na Suluhisho…

Na kaka tatizo halitatuliki, basi unakubaliana nalo na kuangalia namna bora ya kwenda kwa kuanzia hapo ulipo sasa. Weka mpango utakaoufuata na ufuate, kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora zaidi.

Nisichotaka ni kwako wewe rafiki yangu, kukwama mahali, huku akili yako ikikudanganya, halafu baadaye unakuja kustuka muda umekwenda na hujui kipi umefanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.