UKURASA WA 901; Majibu Ya Maajabu…

By | June 19, 2017

Kitu chochote ambacho unataka kujua, kipo hapo ulipo, kipo ndani yako na kipo wazi kabisa mbele yako. Lakini tatizo ni kwamba huamini majibu ambayo unayo, ambayo yako ndani yako, na ambayo yako mbele yako. Badala yake unaamini yapo majibu ya maajabu, majibu ambayo umefichwa na hujawahi kuyaona. Na hivyo unakazana huku na kule kutafuta majibu hayo.

Katika kutafuta huko majibu ya maajabu, ndipo unapokutana na watu wanaokuuzia vitu ambavyo haviwezi kuusaidia, wanaokulaghai na hata kukutapeli. Makosa ni yako kwa kutafuta majibu ya maajabu, wakati majibu ya kweli unayo hapo ulipo.

Ninachokukumbusha rafiki, acha kupoteza muda kutafuta majibu ya maajabu, kutafuta siri zilizofichwa. Hii dunia haina siri kubwa, siri zipo wazi ukishajua wapi pa kuziangalia.

Majibu ya ukweli unayo hapo ulipo,

Unajua kabisa lazima ufanye kazi kwa juhudi na maarifa, kazi ambayo itakuwa ngumu mwanzoni, ambayo itakuchosha na huenda usione manufaa haraka.

SOMA; Unaweza Kutoa Majibu Au Unaweza Kutoa Sababu.

Majibu ya kweli ni kuiendea hofu hata kama inakuwa kubwa kwako, kufanya kile ambacho unahofia hata kama inaonekana haiwezekani. Ni kwa kufanya ndipo unapoishinda hofu, ndipo unapoona fursa zaidi za kufanya vizuri zaidi.

Majibu ya kweli ni kuchagua kile kweli ambacho wewe unaweza na unapenda kukifanya, kuweka juhudi kubwa kukifanya na kujifunza kila siku ili kuboresha zaidi ya kile unachofanya.

Usitafute majibu ya maajabu au muujiza, tengeneza wewe mwenyewe maajabu na muujiza wako, kwa kuweka juhudi kwenye kile ambacho unafanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.