UKURASA WA 906; Jipe Sababu Ya Kujithamini…

By | June 24, 2017

Kuna watu wanajichukia wao wenyewe,

Wapo pia ambao hawajithamini kabisa,

Kwenye kila jambo wanajiona kabisa hawawezi, au wameshashindwa kabla hata hawajaanza.

Hakuna sumu kubwa ya mafanikio kama hii.

Kwa sababu kama hujithamini, hutaweka juhudi kuweza kufanya makubwa. Kwenye kila jambo utajirudisha nyuma wewe mwenyewe.

Kwenye kazi utajiweka nyuma, hutathubutu kusimama na kuomba malipo zaidi. Hili linapelekea wewe kuwa mtu wa chini na kipato kidogo wakati wote.

Kwenye biashara hutaweza kujiamini mbele ya wateja na kuwaeleza kwa hakika kile unachouza na namna kinavyoweza kuwasaidia. Kwa namna hii wateja wanakosa imani kwako na kwa biashara yako. Na hawahamasiki kununua, hata kama unachouza kinawasaidia sana.

SOMA;  Kitu Kimoja Kitakachokujengea Kujiamini Na Kujithamini.

Njia pekee ya kujithamini, ni kujipa sababu ya kujithamini. Sababu ambayo utaikumbuka mara zote unapokuwa kwenye hali ya kutokujithamini.

Jipe sababu ya kuyathamini maisha yako, kwa sababu ya ndoto kubwa za maisha ulizonazo, kwa sababu ya mchango mkubwa ulionao kwa wengine.

Jipe sababu ya kujithamini kwenye kazi yako, kwa sababu ya mchango mkubwa unaotoa kupitia kazi unayofanya, kwa namna kazi yako unavyogusa wengine.

Jipe sababu ya kujithamini kwenye biashara yako, kwa sababu ya bidhaa na huduma nzuri unazotoa, ambazo zinafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi.

Unapojithamini unaweza kufanya zaidi, na unavyofanya zaidi unazidi kujithamini. Hiyo ndiyo inapelekea kwenye mafanikio.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.