Kama umewahi kuangalia tamthilia au maigizo yenye mwendelezo, najua unajua nini huwa kinatokea mwishoni mwa sehemu yenye mwendelezo. Huwa inakuwa ni sehemu nzuri sana, ambayo unataka kujua nini kilitokea? Halafu hapo hapo unaambia litaendelea wakati mwingine au WATCH PART 2.
Unahamasika kusubiri wakati mwingine ili uone nini kilitokea, au unaenda kununua sehemu inayoendelea ili ujue nini hasa kilitokea. Kwa kitu rahisi kama hivyo, ambacho hata siyo kweli, ni igizo pekee, wengi wanakazana sana kuhakikisha wanachukua hatua kujua nini kitaendelea.
Na sisi pia tunaweza kutumia nguvu hiyo katika kuhakikisha tunafanya makubwa kwenye maisha yetu. Kama kuna kazi tunafanya, ambayo inabidi kuendelea wakati mwingine, basi achia pale patamu. Achia sehemu ambayo unapokuja kuweka juhudi kidogo tu unapata matokeo makubwa sana. kwa njia hii utahamasika kurudi kwenye kazi hiyo muda wa kurudi unapofika.
SOMA; Maisha Yako Ni Kazi Inayoendelea….
Hata kama ni kitabu unasoma, unapopanga kuahirisha ili uendelee kusoma wakati mwingine, ishia sehemu ambayo ni nzuri na ungependa kujua nini kitakachofuata. Kisha nenda na ratiba zako nyingine, utakapofika wakati wa kuendelea kusoma, utarudi kusoma kwa hamasa ili kuendelea kujifunza pale ulipoishia.
Tumia kila njia kuhakikisha hamasa ya kurudi kufanya jambo inakuwa kubwa kuliko hamasa ya kuahirisha.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog