Najua hiyo ni kauli tata unayoweza kuisikia kutoka kwa mtu kama mimi, ambaye kila wakati nakuandikia kuhusu maisha ya mafanikio. Niruhusu nikufafanulie hili vizuri, ili unapoendelea kutafuta mafanikio, ujue yapi muhimu ya kuzingatia.
Umewahi kusikia watu wakisema mtu fulani ana bahati sana? labda kuna kitu kimetokea na yeye pekee ndiyo akawa anafaa kwa kile kilichotokea, labda ni fursa au nafasi muhimu, ambayo imemwangukia yeye tu. Ni kweli zipo hali za aina hiyo, lakini unapochimba ndani zaidi, unaona siyo kwamba bahati zimewaangukia tu, ila walizikaribisha bahati hizo.
Ndiyo maana nakuambia, mafanikio hayatengenezwi, bali yanavutiwa. Huwezi kuyatengeneza mafanikio, bali unayavutia mafanikio.
Unayavutia mafanikio kwa namna ambavyo unayajenga maisha yako, katika misingi ya NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA, unatengeneza maisha ambayo mafanikio yanakuja kwako. Watu kwa nje wataona una bahati, ila kwa ndani unajua ni namna gani umeweka juhudi na kujinyima vitu vizuri ili upate bora.
SOMA; Kikwazo Cha Elimu Kubwa Kwenye Mafanikio Ya Biashara….
Wote tunajua kwama, maisha yetu hayawezi kubadilika kama sisi wenyewe hatutabadilika.
Tunajua ili kitu chochote kifanye kazi, lazima sisi wenyewe tufanye kazi kwanza.
Tunajua ili vitu viwe bora, lazima sisi tuwe bora kwanza.
Na hii ndiyo maana ni muhimu uelewe kwamba, maisha unayotengeneza, ndiyo yanavutia au kufukuza mafanikio yako.
Badala ya kukimbiza mafanikio kama wengi wanavyofanya, wakiamini yanapatikana maeneo fulani pekee, wewe tengeneza maisha ambayo yatavutia mafanikio popote pale ulipo, kwa lolote ulilochagua kufanya.
Ishi maisha ambayo yatavutia mafanikio.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog