Dunia inaendeshwa kwa msingi mmoja muhimu sana, mabadiliko ni muhimu na yanatokea kila wakati. Hivyo jambo muhimu sana ambalo mtu unaweza kufanya, ni kubadilika, kila siku japo kwa hatua ndogo sana.
Wale wote ambao wamekuwa hawataki kubadilika, wamekuwa wanaachwa nyuma. Wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea, kitu ambacho kinawarudisha nyuma.
Ili kuweza kufanya kazi bora, kuweza kutoa kitu chenye thamani zaidi kwa wengine, ni lazima ubadili kitu unafanya. Ni lazima uweke ubora zaidi, ni lazima uweke ubunifu, na haya yote yanakutaka wewe ubadilike kwanza.
Lakini jambo ambalo limekuwa linashangaza, ni namna gani watu wanataka mabadiliko, ila wao wenyewe hawapo tayari kubadilika. Wanapenda kuona matokeo bora ila waendelee na maisha yao kama yalivyo sasa. Kitu ambacho hakiwezekani kwa namna yoyote ile.
SOMA; Usiwe Mmoja Kati Ya Hawa…
Hivyo, leo nakukumbusha rafiki, kama huna mpango wowote wa kubadili kitu leo, ni bora urudi ukalale, kwa sababu unakwenda kuipoteza siku ya leo. Unapojaribu kwenda kuifanyia kazi siku ya leo kwa mazoea, unakwenda kupata matokeo mabovu kuliko jana. Japo wewe unaona umepata kama jana, kumbuka dunia inasonga mbele. Hivyo kama unapata sawa na jana, na dunia imesonga mbele kidogo leo, unafikiri wewe utakuwa wapi? Nyuma.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog