UKURASA WA 997; Kazi Zetu Ni Watu…

By | September 23, 2017

Kwenye kila kitu ambacho tunafanya hapa duniani, kinawahusisha watu wengine. Iwe umeajiriwa au unafanya biashara, unachofanya ni kwa ajili ya watu na unakifanya na watu. Hata katika maisha yetu ya kawaida, mahusiano yetu yanahusisha watu.

Hivyo tunaweza kusema kwamba kila mmoja wetu, kazi yake kubwa ni watu. Katika kazi hii, tuna majukumu makuu mawili;

Jukumu letu la kwanza ni kuwatendea wema. Kufanya kile ambacho tunafanya kwa njia ya kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi, kuwapa thamani zaidi.

Jukumu letu la pili ni kuwachukulia kwa jinsi walivyo. Hapa tunahitaji kuwavumilia wengine na kuchagua kwenda nao kwa namna walivyo.

Ukiona

Pamoja na majukumu hayo mawili, ambayo yote ni mema kwa wengine, bado watu hao ndiyo changamoto kubwa kwetu. Watu hawa ambao ndiyo kazi yetu kuu, wanaifanya kazi hiyo iwe ngumu, japo tunaifanya kwa manufaa yao.

Upo wakati wale ambao umejitoa kwa ajili yao, wanafanya maisha yawa magumu mno. Unaweza kuwa umejitoa kabisa kuhakikisha maisha ya wengine yanakuwa bora, lakini wale unaowakazania wakawa ndiyo wa kwanza kukataa na kukupinga kwa kile unachofanya.

SOMA; UKURASA WA 133; Neno Lako Kama Sheria.

Pamoja na hayo yote, tunapaswa kukumbuka jambo moja muhimu, ugumu ndiyo njia yenyewe. Pale ambapo unakutana na changamoto, lazima ujue changamoto hiyo ni sehemu ya njia. Lazima uitatue ndiyo uweze kusonga mbele.

Endelea kutekeleza majukumu yako makuu mawili kwenye kazi yako kuu ambayo ni watu. Wapo watakaokuelewa na kunufaika na wapo ambao hawatakuelewa na kukupinga. Kadiri unavyoendelea kufanya ndivyo wengi zaidi watanufaika na kukuelewa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.