Maisha yetu wanadamu kuna wakati yanakuwa ya ajabu sana.
Mtu unakazana kutafuta na kupata vitu, halafu ukishavipata vinakuwa matatizo kwako.
Umewahi kukutana na mtu ambaye maisha yake yalikuwa mazuri kabla hajapata fedha au utajiri, lakini baada ya kupata vitu hivyo maisha yanakuwa magumu?
Wengi wamekuwa wakisema kabisa kwamba ni bora kuwa na maisha madogo ya kawaida, kwa sababu yana amani, kuliko kuwa na maisha makubwa na ya mafanikio ambayo kila wakati yana wasiwasi.
Ukweli ni kwamba, hakuna kinachobadilika kama tuna mali nyingi au hatuna, bali fikra zetu na matamanio yetu ndiyo vinaharibu kila kitu.
Ni kawaida kwetu binadamu kujishikiza na vitu, tunaona ni vitu vyetu, tunastahili kuwa navyo na mbaya zaidi, tunaona maisha yetu hayawezi kwenda kama hatuna vitu hivyo.
Sasa mtu anapofikia hatua ya kuona maisha hayawezi kwenda mpaka awe na vitu fulani, ameshapoteza uhuru kwenye vitu hivyo na vitamtesa.
Kwanza atakazana kuwa na vyo hata kwenye mazingira ambayo hayaruhusu, kitu kitakachomuumiza.
Pili akipoteza vitu hivyo mambo yanakuwa magumu zaidi kwake, kwa sababu anaona maisha kama hayawezekani tena.
Wanafalsafa wa Ustoa walijua hatari hii mapema kabisa, na kutengeneza njia ambayo itawaepusha kuona maisha yao hayafai pale wanapopoteza kile walichonacho.
Hivyo walijipa mazoezi ya kufanya vitu ambavyo ni tofauti na mali walizonazo. Kwa mfano mtu kuchagua kulala chini mara moja moja licha ya kuwa na kitanda, au kuona maji ya kunywa na kuyamwaga wakati ana kiu kali.
SOMA; FALSAFA MPYA YA MAISHA; Njia Ya Uhakika Ya Kuwafanya Watu Wakupe Kile Unachotaka.
Mara kwa mara, jaribu kuishi bila ya kile unachofikiri kwamba huwezi kuishi bila ya kuwa nacho. Utaona namna gani maisha yanawezekana na utaacha kujishikiza na vitu hivyo na kuwa na uhuru na maisha yako.
Muhimu, huku siyo kujitesa kama wengi wanavyoweza kuchukulia, bali ni kutengeneza uhuru mkubwa wa maisha yako, uhuru usioharibiwa na kitu chochote.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog
Pingback: UKURASA WA 1101; Uhuru, Uvumilivu Na Nguvu Ni Zao La Kitu Hichi Kimoja… – Kisima Cha Maarifa