#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jinsi ya kufufua na kuchochea udadisi. KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 57 – 66. Watoto wadogo huwa wanakuwa na maswali mengi sana. Huwa wanahoji na kudadisi kila kitu. Lakini kadiri wanavyokua, ndivyo udadisi wao unavyopungua. Maswali yanaisha na wanakubaliana na majibu wanayoyapata au kile wengine amekubali. Hali hii wanakuwa wamejifunza, kutokana na majibu waliyopokea wakati wa udadisi na maswali mengi. Huenda ni kukatishwa tamaa au kukemewa na kuambiwa waache usumbufu. Kila mtu anaweza kufufua na kuchochea udadisi ambao upo ndani yake. Na njia ya kufanya hivyo ni kuanza kuhoji maswali. Kuanza kuhoji kila kitu na kuchunguza kwa kina. Badala ya kukubaliana na majibu rahisi yanayotolewa na kukubaliwa na wengine, unahitaji kuhoji zaidi. Zoezi hili kinakuwa bora zaid kama ukiwa na kijitabu cha kuandika maswai uliyonayo. Hapa unaandika yale maswali unayojiuliza au kudadisi chochote unachokutana nacho. Leonardo da Vinci anasifika kwa kuwa na vijitabu vingi ambavyo alikuwa akiandika maswali yake. Kila alichohoji na kudadisi alikiandika, na hili lilimwezesha kupiga hatua zaidi. Njia bora zaidi ya kuhakikisha unahoji maswali muhimu ya udadisi ni zoezi la maswali 100. Hapa unajihoji na kuandika maswali 100 muhimu zaid kwako. Maswali haya hayahitaji kuwa na umaalumu wowote, bali ni kuihoji akili yako mpaka itoe maswali 100. Zoezi hili litakuwezesha wewe kujijua kwa undani na kujua kile hasa unachoamini na hata kujali pia. Mara zote kuwana kijitabu, na mara zote hoji na dadisi, utajifunza mengi sana. Rafiki na Kocha wako, Dr. Makirita Amani, www.amkamtanzania.com/kurasa

By | November 6, 2017
KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 57 – 66. Watoto wadogo huwa wanakuwa na maswali mengi sana. Huwa wanahoji na kudadisi kila kitu. Lakini kadiri wanavyokua, ndivyo udadisi wao unavyopungua. Maswali yanaisha na wanakubaliana na majibu wanayoyapata au kile wengine amekubali. Hali hii

MUHIMU; Ili kuendelea kusoma makala hii unahitaji uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kama tayari ulishajiunga na kuwa mwanachama weka taarifa zako kwenye sehemu ya LOG IN kwenye fomu hapo chini.. Kama bado hujajiunga na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza sehemu iliyoandikwa Click here to register na utapata maelekezo pamoja na kujiandikisha.

Existing Users Log In
   
Category: #KURASA_KUMI ZA KITABU KILA SIKU

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz