Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

3314; Muda na usumbufu.

By | January 27, 2024

3314; Muda na usumbufu. Rafiki yangu mpendwa, Imekuwa ni kawaida kwa watu kusema kama wangepata muda zaidi basi wangeweza kufanya makubwa. Hiyo imekuwa ni njia nyingine ya watu kuonyesha kwamba kinachowakwamisha ni ufinyu wa muda. Lakini tunajua ukweli kwamba muda uliopo ni sawa kwa kila mtu.Kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza (more…)

3313; Kwa nini juhudi zako hazizai matunda.

By | January 26, 2024

3313; Kwa nini juhudi zako hazizai matunda. Rafiki yangu mpendwa,Ukiwaangalia wale wanaoshindwa na wanaofanikiwa, huwezi kuona tofauti kubwa sana kwa nje.Kwa sababu kama ni juhudi, wote wanaweza kuonekana wakiweka juhudi kubwa.Tena wakati mwingine wanaoshindwa wataonekana wanaweka juhudi kubwa kuliko hata wale wanaofanikiwa. Lakini bado juhudi hizo kubwa wanazokuwa wanaweka hazizai (more…)

3312; Hatua na matokeo.

By | January 25, 2024

3312; Hatua na matokeo. Rafiki yangu mpendwa, Matokeo tunayoyapata mwenye maisha yanatokana na hatua tunazochukua.Lakini watu wengi huwa wanasahau hilo na kuyaangalia matokeo yenyewe.Na kama matokeo hayawafurahishi, hawajitathmini kwenye hatua walizochukua, bado wanaangalia nini kingine wafanye ili kupata matokeo wanayotaka. Mara nyingi sana, pale mtu anapokosa matokeo aliyokuwa anayataka, mahali (more…)

3311; Tatizo sahihi na kazi.

By | January 24, 2024

3311; Tatizo sahihi na kazi. Rafiki yangu mpendwa, Tamaa ya kupata mafanikio makubwa kwa njia za mkato ni kitu ambacho hakijawahi kuisha kwa watu.Kwenye kila zama huwa kunakuwa na njia za mkato ambazo huwa zinaibuliwa na kuonekana ni njia bora ya kufanikiwa bila kuweka kazi.Lakini njia hizo hazijawahi kufanya kazi. (more…)

3310; Msukumo wa kufanya.

By | January 23, 2024

3310; Msukumo wa kufanya. Rafiki yangu mpendwa, Huwa kuna kauli inayosema hatima ya yai ni kuvunjika.Na matokeo ya kuvunjika kwa yai huwa yanategemea chanzo cha nguvu ya kuvunja yai hilo.Kama yai litavunjwa kwa nguvu inayotoka nje, huwa ni mwisho wa uhai wake.Lakini kama yai litavunjwa kwa nguvu inayoanzia ndani, huwa (more…)

3309; Okoa hizo nguvu.

By | January 22, 2024

3309; Okoa hizo nguvu. Rafiki yangu mpendwa, Moja ya kanuni za fizikia ni uhifadhi wa nguvu.Kanuni hiyo inasema nguvu haiwezi kutengenezwa wala kuharibiwa, bali inaweza kubadilishwa kutoka hali moja kwenda nyingine. Kanuni hii inagusa kila eneo la maisha yetu, hasa kwenye miili yetu.Kama unakosa nguvu za kuyapambania mafanikio yako, siyo (more…)

3308; Usiende kinyume.

By | January 21, 2024

3308; Usiende kinyume. Rafiki yangu mpendwa, Kinachofanya watu wengi kushindwa kupata mafanikio makubwa ambayo yapo ndani ya uwezo wao ni kwenda kinyume na vile wanavyopaswa kwenda. Yaani unakuta mtu tayari yupo kwenye njia sahihi ya kufanikiwa, lakini anachagua kwenda kinyume na vile anavyopaswa kwenda ili kufanikiwa au kudumu kwenye mafanikio. (more…)

3307; Chagua kwa usahihi.

By | January 20, 2024

3307; Chagua kwa usahihi. Rafiki yangu mpendwa,Wakati mwingine watu wanashindwa kwenye kile wanachofanya, siyo kwa sababu hakiwezekani, bali kwa sababu wanakuwa hawajachagua kwa usahihi wale wanaowalenga. Unaweza kuwa na biashara ambayo ni nzuri kabisa, ambapo kuna thamani kubwa unayoitoa, ambayo watu wana uhitaji nayo, lakini bado ikashindwa.Biashara kama hiyo inashindwa (more…)

3306; Kukubali kuwa kawaida.

By | January 19, 2024

3306; Kukubali kuwa kawaida. Rafiki yangu mpendwa, Watu wengi wamekuwa kawaida kwenye maeneo yote ya maisha yao, kitu ambacho kinawafanya wasipate mafanikio makubwa ambayo wangeweza kuyapata. Kinachosababisha hilo ni wao kutaka kufanya kila kitu, kudhani wanaweza kuwa bora kwenye vitu vyote.Hapo wanagawa rasilimali zao kwa usawa kwenye mambo mengi wanayofanya. (more…)