Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

3195; Kuwa mchezaji hatari kwenye mashindano.

By | September 30, 2023

3195; Kuwa mchezaji hatari kwenye mashindano. Rafiki yangu mpendwa,Kama tukiyachukulia maisha kama mchezo na wewe kama mchezaji, unaweza kuwa mchezaji hatari sana kwenye hayo mashindano.Utakuwa na hatari pale unapokuwa unaanzia chini kabisa na huna chochote cha kupoteza. Kwenye mashindano ya aina yoyote ile ni wachezaji wanaoanzia chini kabisa na hawana (more…)

XXII; Kuhusu ubatili wa kuwa njia panda.

By | September 29, 2023

XXII; Kuhusu ubatili wa kuwa njia panda. Rafiki yangu Mstoa, Kufanya maamuzi na kuyasimamia kwenye utekelezaji ni kitu ambacho kimekuwa changamoto kwa watu wengi.Kwa kutaka matokeo fulani, watu hufanya maamuzi sahihi.Lakini inapokuja kwenye utekelezaji, huwa wanasita kuchukua hatua zinazopaswa kuchukuliwa kulingana na maamuzi waliyofanya.Hapo watu wanakuwa njia panda, kwa sababu (more…)

3194; Sehemu ngumu zaidi kwenye mipango.

By | September 29, 2023

3194; Sehemu ngumu zaidi kwenye mipango. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi huwa hawapati mafanikio makubwa kwenye maisha yao.Na siyo kwa sababu hawataki kufanikiwa, wanakuwa wanataka sana.Pia siyo kwa sababu hawaweki mipango ya kufanikiwa, wanaiweka sana tu.Na pia siyo kwamba hawaanzi kufanyia kazi mipango yao, huwa wanaanza wakiwa na shauku kubwa.Lakini sasa, (more…)

3193; Ndiyo sababu ya kufanya.

By | September 28, 2023

3193; Ndiyo sababu ya kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Karibu kila mtu anajua nini hasa anachotaka kwenye maisha yake.Na pia wengi wanajua nini wanapaswa kufanya ili kupata wanachotaka.Lakini cha kushangaza, inapokuja kwenye kufanya, wengi huwa hawachukui hatua. Tunaweza kushangaa kwa nje, iweje watu washindwe kufanya kile wanachojua kabisa kwamba wanapaswa kufanya ili (more…)

3192; Maarifa, Maadili na Ujuzi.

By | September 27, 2023

3192; Maarifa, Maadili na Ujuzi. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye ukurasa uliopita wa 3191 tumejifunza kuhusu Ujuzi, Tabia Na Muda.Kwenye ukurasa huu tunakwenda kupata toleo la watoto la vitu vitatu muhimu kuwajengea ili kuwaandaa kwa maisha ya mafanikio. Lakini kabla ya kuingia kwenye ukurasa huu, nianze kwa kuambiana ukweli sisi kama wazazi.Wengi (more…)

3191; Ujuzi, Tabia Na Muda.

By | September 26, 2023

3191; Ujuzi, Tabia Na Muda. Rafiki yangu mpendwa,Hali ya watu kutafuta njia ya mkato ya kupata mafanikio halijaanza leo na wala halitaisha leo.Tangu enzi na enzi watu wamekuwa wanatafuta hizo njia za mkato.Lakini kwa bahati mbaya sana, wamekuwa wanaishia kupoteza nguvu, fedha na muda.Haijawahi kuwepo njia ya mkato ambayo inampa (more…)

3190; Unachokosea kwenye msimamo.

By | September 25, 2023

3190; Unachokosea kwenye msimamo. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vitu ambavyo tumekuwa tunasisitizana sana kwenye hii safari yetu ya mafanikio makubwa ni msimamo.Ambapo ni kufanya bila ya kuacha, liwake jua au inyeshe mvua.Bila ya kufanya jambo kwa msimamo bila ya kuacha, huwezi kupata mafanikio makubwa. Wapo watu wanasikia hili la msimamo (more…)

3189; Unaanza na kufanya.

By | September 24, 2023

3189; Unaanza na kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Kinachowakwamisha watu wengi kupata kile wanachotaka kwenye maisha yao ni kushindwa kuelewa jinsi mipango, hamasa na ufanyaji vinavyohusiana. Hivyo wengi huwa wanatumia muda wao mwingi kupanga nini watafanya. Na hata baada ya kupanga, bado wanatumia muda mwingi kupitia mipango waliyojiwekea. Halafu wanakuja kusubiri mpaka (more…)

3188; Ni milioni tu.

By | September 23, 2023

3188; Ni milioni tu. Rafiki yangu mpendwa,Mwenzetu hapa, Martin Tindwa, anaandika kitabu ambacho anakiita Jilipe Wewe Mwenyewe. Ni kitabu kuhusu mpango binafsi wa kifedha wa kujilipa wewe mwenyewe kwanza kwenye kila kipato ambacho mtu unaingiza. Kwenye kitabu hicho, Martin kuna dhana moja muhimu sana ambayo ameizungumzia na ina uzito mkubwa (more…)