Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

3305; Jiamini, amua.

By | January 18, 2024

3305; Jiamini, amua. Rafiki yangu mpendwa, Kila mtu kwenye maisha anajua nini hasa anachotaka kupata na nini hasa anachopaswa kufanya ili kupata anachotaka. Hayo yapo wazi kabisa kwa mtu, lakini kwa nje inaweza kuonekana tofauti.Kwa nje watu wengi wanaonekana kama hawajui nini wanataka na nini wanapaswa kufanya ili kupata matokeo (more…)

3304; Kukwepa kuwajibika.

By | January 17, 2024

3304; Kukwepa kuwajibika. Rafiki yangu mpendwa,Unakumbuka ulipokuwa mdogo na ukatamani sana kuwaonyesha watu jinsi unavyoweza kufanya mambo yanayofanywa na watu wazima.Na baada ya kufanya hivyo yakageuka kuwa sehemu ya majukumu yako.Yaani baada ya kuonyesha kwamba unaweza, ukaanza kupangiwa uyatekeleze. Ni hali hiyo ya kuwajibika ndiyo imekuwa inapelekea watu wengi kutokuwa (more…)

3303; Wa kumfuata mwenzake.

By | January 16, 2024

3303; Wa kumfuata mwenzake. Rafiki yangu mpendwa, Pale unapokuwa unashirikiana na watu wengine, na wewe ukawa uko mbele zaidi ya hao wengine, huwa unafanya nini ili muweze kwenda pamoja? Kwa walio wengi huwa wanapunguza kasi yao na kuwasubiri hao wengine ili waambatane nao.Hapo wanakuwa wameshusha viwango vyao ili kuweza kueleweka (more…)

3302; Kujidanganya kwenye fedha.

By | January 15, 2024

3302; Kujidanganya kwenye fedha. Rafiki yangu mpendwa,Hakuna watu ambao huwa wanajidanganya kwenye fedha kama wale ambao hawana fedha nyingi.Huwa wanajidanganya kama sehemu ya kujifariji.Lakini kujidanganya huko bado huwa hakuondoi ukweli kwamba hawana fedha na fedha ni muhimu. Fedha ni muhimu sana kwenye maisha, kwa sababu inanunua vitu vingi tunavyohitaji kwenye (more…)

3301; Kupata na kukosa.

By | January 14, 2024

3301; Kupata na kukosa. Rafiki yangu mpendwa, Kuna watu huwa wanadhani maisha yanaendeshwa kwa bahati.Kwamba wenye bahati wanapata wanachotaka na wasiokuwa na bahati wanakosa. Lakini ukweli ni kwamba maisha yanaendeshwa na kupata au kukosa.Ni labda unapata kile unachotaka au unakikosa. Ili upate unachotaka, lazima kuna juhudi unazopaswa kuweka.Ni pale watu (more…)

3300; Ambacho huwezi kupata.

By | January 13, 2024

3300; Ambacho huwezi kupata. Rafiki yangu mpendwa, Wakati tupo shule tulikuwa na usemi mmoja kwamba unapoenda kwenye sherehe au mtoko wowote unaohusisha chakula, basi unapaswa kula chakula ambacho ni tofauti na kile unachokula kila siku. Kwa sababu hicho cha kila siku unajua utaendelea kula, hivyo ni bora kutumia fursa mpya (more…)

3299; Uhakika wa kushinda au kushindwa.

By | January 12, 2024

3299; Uhakika wa kushinda au kushindwa. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye maisha, kushinda au kushindwa ni vitu ambavyo mtu anachagua mwenyewe.Hayo huwa siyo matokeo ya nje kama wengi wanavyodhani.Bali ni maamuzi ya ndani ya mtu mwenyewe. Mtu anakuwa na uhakika wa kushindwa pale;1. Anaposema anajaribu kufanya kitu. Kujaribu kufanya kitu ni (more…)

3297; Uko sahihi kabisa.

By | January 10, 2024

3297; Uko sahihi kabisa. Rafiki yangu mpendwa, Kwenye hii safari ya kujifunza, kufundisha na kukochi watu kwenye eneo la mafanikio, naendelea kujifunza mengi sana. Moja ya hivyo ninavyojifunza ni mtazamo hasi ambao watu wengi wanao kwenye kupata mafanikio. Imekuwa ni imani yangu na nguzo kuu ya mafundisho yangu kwamba kila (more…)

3296; Hakuna kingine muhimu.

By | January 9, 2024

3296; Hakuna kingine muhimu. Rafiki yangu mpendwa, Sababu namba moja ya watu wengi kushindwa kupata matokeo makubwa waliyokuwa wanayataka ni kutawanya nguvu zao kwenye mambo mengi. Wanakuwa wanapambania vitu vingi kwa wakati mmoja, kitu ambacho kinapunguza ufanisi wao.Kwa sababu hata kama watapata matokeo, yanakuwa ni ya kawaida sana. Matokeo makubwa (more…)