Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Maswali Matatu Muhimu Kujiuliza Kuhusu Wateja Wa Biashara Yako.

By | October 3, 2017

Mambo yanabadilika kwa kasi sana, na biashara nazo hazijaachwa nyuma. Kuweza kupona kibiashara kwenye zama hizi za mabadiliko, lazima uwe mbele ya mabadiliko. Lazima uweze kubadilika kabla mabadiliko hayajafika. Tabia za watu zinabadilika sana kwa sasa, na hii inakufanya wewe mfanyabiashara kuzielewa tabia za wateja wako, ili uweze kuwahudumia vizuri (more…)

BIASHARA LEO; Ushauri Bora Kabisa Wa Biashara Yako Upo Kwenye Tabia Za Wateja Wako…

By | September 29, 2017

Unapokuwa na wateja ambao wanalalamikia mambo mengi kwenye biashara yako, ni vyema ukajihakikishia kwamba ni wateja sahihi kabla hujachukua hatua. Kwa sababu wapo watu ambao wamepewa ushauri wa namna ya kuboresha biashara zao na watu ambao siyo wateja wa biashara hizi. Yaani mtu anakuja na kukuambia ungefanya hivi ungepeta wateja (more…)

BIASHARA LEO; Weka Roho Yako Kwenye Biashara Yako.

By | September 27, 2017

Najua unajua kwamba utandawazi umeifanya dunia kuwa kijiji. Kila siku dunia inazidi kuwa ndogo zaidi na zaidi. Na hili limekuwa na madhara makubwa sana kwenye biashara. Kwa mfano, siku za nyuma watu walifikiri ukishakuwa na biashara yako eneo fulani na ukaweza kuikuza pale, basi hakuna kinachoweza kukuhatarisha kama utakuwa mwangalifu (more…)

BIASHARA LEO; Huuzi Tu Biashara, Unajiuza Na Wewe Pia.

By | September 25, 2017

Katika kununua, watu wanaendeshwa na hisia zaidi ya fikra. Huwa tunafikiri kwamba watu watakuwa ‘logical’ katika kufanya maamuzi ya kununua, lakini huo siyo ukweli. Watu huwa wanaendeshwa na hisia zaidi katika kufanya maamuzi kuliko kufikiri kwa kina. Na hapo ndipo wengi wanapokosea, kwa kuamini watu watanunua kile wanachouza, kwa sababu (more…)

BIASHARA LEO; Kazi Yako Siyo Kuwaambia Watu Kipi Wanataka, Bali Kuwasikiliza Nini Wanataka.

By | September 22, 2017

Mapinduzi makubwa sana yameshafanyika kwenye biashara kwa ujio wa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii. Sasa hivi nguvu kubwa ipo kwa wateja na siyo wafanyabiashara. Siku za nyuma ilikuwa kampuni inaamua izalishe nini, kisha inatengeneza matangazo yenye kuvutia sana na kuwashawishi watu mpaka wapokee ile bidhaa inayotolewa. Lakini sasa (more…)

BIASHARA LEO; Watu Hawapendi Kuuziwa, Bali Wanapenda Kununua.

By | September 21, 2017

Hii ni dhana ambayo itakusaidia sana kubadili mtazamo wako kibiashara, hasa pale unapokutana na mteja wako. Japokuwa upo kwenye biashara kuuza bidhaa na huduma unazotoa, kumbuka kwamba mteja haji kwako kwa sababu wewe unauza. Bali mteja anakuja kwako kwa sababu ana shida au changamoto, na ana amini ya kwamba wewe (more…)

BIASHARA LEO; Bidhaa Bora Haihitaji Punguzo La Bei…

By | September 20, 2017

Moja ya mjadala mkubwa kwenye biashara, hasa biashara ndogo ni iwapo mtu unaweza kuvutia wateja zaidi kwa kuweka punguzo la bei, au kuuza bei rahisi kuliko wengine. Na mara nyingi majibu ni ndiyo ndani ya muda mfupi, utavutia wateja ndani ya muda mfupi, lakini iwapo na wengine nao watapunguza bei, (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Mmoja Asikufanye Ubadili Biashara Yako Yote…

By | September 19, 2017

Wakati unapoanza biashara yoyote, huwa unakuwa na mawazo yako juu ya biashara hiyo. Huwa unakuwa na mipango mikubwa juu ya biashara yako na wateja unaowalenga pia. Lakini unapoingia kwenye biashara hasa, mambo huwa tofauti na ulivyotegemea. Wakati mwingine kitu ulichofikiri wateja wanakitaka kweli kinakuwa siyo kitu chenyewe. Hili linakufanya ubadili (more…)

BIASHARA LEO; Mahitaji Binafsi Na Mahitaji Ya Wengine Kwenye Biashara…

By | September 18, 2017

Zipo biashara ambazo huwa zinaanza kwa hamasa na nguvu kubwa. Biashara hizo zinakua kwa kasi sana, watu wanapata mahitaji yao na wanaridhishwa sana. Lakini baada ya muda, biashara hizi zinaacha kuwapendeza watu, zinatoa huduma mbovu na watu kuzikimbia. Yapo mengi yanayoweza kusababisha hali ya aina hii kwenye biashara, lakini kubwa (more…)

BIASHARA LEO; Tengeneza Mfumo Wa Biashara Moja Kusimama Kabla Hujaenda Nyingine…

By | September 15, 2017

Tunaishi kwenye dunia ya wingi, kila mtu anapenda kuwa na vitu vingi. Kwa sababu dunia inachanganya wingi na mafanikio. Kwamba mwenye vingi ndiye aliyefanikiwa, asiyekuwa na vingi basi ameshindwa. Hii ni falsafa mbovu sana kwenye kila eneo la maisha. Lakini inakuwa mbovu zaidi inapoingia kwenye biashara. Wapo watu wanapima mafanikio (more…)