Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Jua Eneo Hili La Biashara Yako Linalokurudisha Nyuma.

By | September 14, 2017

Biashara yenye mafanikio inaendeshwa kwa mfumo. Mfumo wa biashara unakuwa na vipengele mbalimbali kama mauzo, masoko, uzalishaji, usimamizi na kadhalika. Kwa njia hii ya mfumo, mmiliki wa biashara anaweza kuiendesha vizuri biashara yake na kwa mafanikio makubwa sana. Lakini mifumo yote ina changamoto kubwa moja, eneo moja likiwa na changamoto, (more…)

BIASHARA LEO; Hebu Tukumbushane Tena Kwa Nini Unapaswa Kuwa Na Biashara…

By | September 13, 2017

Nimekua nakuambia hili mara kwa mara, na leo nakukumbusha tena kwamba siyo lazima kila mtu ajiajiri na kuwa na biashara. Lakini kila mtu anapaswa kuwa na mifereji mingi ya kipato, hasa kwa walioajiriwa. Kutegemea mshahara pekee kama njia kuu ya kipato, ni hatari mno, kama ambavyo kila mtu amekuwa anaona (more…)

BIASHARA LEO; Usiogope Kuwasumbua Wateja…

By | September 11, 2017

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanatumia sababu za ajabu sana kuendesha biashara zao kwa uzembe. Moja ya sababu hizo ni kuogopa kuwasumbua wateja. Wapo wafanyabiashara ambao wamekuwa wanapoteza wateja kwenye biashara zao, kwa sababu wanaogopa kuwasumbua. Labda ni kumkumbusha mteja kuja tena kwenye biashara, wengi huona wakifanya hivyo mteja ataona ni kama (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Watu Hawajanunua Wanataka Hichi, Na Baada Ya Kununua Wanataka Hichi.

By | September 7, 2017

Sehemu muhimu sana ya biashara ni mauzo, bila ya mauzo, biashara yoyote inakufa, hata kama ni nzuri kiasi gani. Pamoja na maeneo yote ya biashara kuwa muhimu, eneo la mauzo linahitaji mtazamo wa kipekee ili kuhakikisha biashara inaendelea kwenda. Katika kuuza, watu wengi hufanya makosa, ya kujiangalia wao wenyewe badala (more…)

BIASHARA LEO; Sehemu Ngumu Zaidi Ya Biashara Siyo Biashara Yenyewe, Bali Watu.

By | September 6, 2017

Kuendesha biashara kuna changamoto nyingi sana. Changamoto hizi zimewazuia wengi kuweza kukuza biashara zao na kufikia mafanikio makubwa. Changamoto hizi za biashara tunaweza kuzigawa kwenye makundi makuu mawili. Changamoto za kibiashara na changamoto za watu. Changamoto za kibiashara hizi ni zile za kawaida, mauzo, mzunguko wa fedha, mwenendo wa uchumi, (more…)

BIASHARA LEO; Nenda Zaidi Ya Matatizo Na Mahitaji.

By | September 5, 2017

Unapoanzisha biashara, kitu kikubwa ni kuangalia matatizo au changamoto ambazo watu wanazo, kisha unakuja na suluhisho la matatizo na changamoto hizo. Hilo ndilo ambalo kila mfanyabiashara anafanya. Na kwa kuwa huna cha kuwazuia watu kufanya unachofanya wewe, kutegemea hilo pekee hakukuwezeshi kuwa na wateja waaminifu kwa biashara yako. Wateja waaminifu (more…)

BIASHARA LEO; Anza Na Kitu Ambacho Watu Tayari Wanakihitaji.

By | September 4, 2017

Kwenye kitabu cha The Lean Startup, mwandishi Erick Ries anatushirikisha dhana ya MVP ambayo kirefu chake ni Minimum Viable Product. Dhana hii inaeleza kwamba unapoanza biashara, anza na bidhaa ambayo haujakamilika, lakini iwe na sifa ambazo inaweza kumsaidia mtu. Badala ya kutumia nguvu nyingi kuja na bidhaa au huduma kamili, (more…)

BIASHARA LEO; Kosa Kubwa Wanalofanya Wanaoanza Biashara…

By | September 3, 2017

Upo usemi kwamba mwanzo ni mgumu, na usemi huu unafanya kazi kwenye kila jambo, kuanzia ukuaji wetu mpaka shughuli zetu. Pata picha ya mtoto mdogo ambaye anajifunza kutembea, anasimama na kuanguka, anapiga hatua moja anaanguka. Lakini mtoto huyu hasemi kutembea ni kugumu basi naachana nako. Bali anaendelea na baada ya (more…)

BIASHARA LEO; Katika Mipango Yako Ya Biashara, Mteja Ni Sehemu Muhimu…

By | September 2, 2017

Mara nyingi watu wanapoweka mipango yao ya kibiashara, hujiangalia wao zaidi. Hili huanzia kwenye kufikiria biashara ya kufanya, wengi hufikiria kile ambacho wanapenda wao, na kwenda nacho kwa njia ambayo wanaitaka wao. Pia katika mabadiliko ya kibiashara, wengi hujiangalia wao. Kwa mfano katika maamuzi ya kubadili bei au kubadili huduma (more…)

BIASHARA LEO; Aina Mbili Za Uchumi Wa Biashara Na Ipi Ya Kuwekea Mkazo…

By | September 1, 2017

Zipo aina mbili za uchumi wa biashara, aina moja ni rahisi kufanya lakini matokeo yake siyo mazuri. Aina nyingine ni ngumu kufanya lakini matokeo yake ni mazuri, hasa ukiweza vizuri. Aina ya kwanza ni kuwafikia wateja wengi uwezavyo, kukazana kila mtu awe mteja wako. Hapa inakubidi uwe na kitu ambacho (more…)