Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Mteja Mmoja Baada Ya Mwingine…

By | July 27, 2017

Kosa kubwa ambalo wafanyabiashara wapya wamekuwa wanafanya ni kutaka siku ya kwanza ya biashara wawe na wateja wengi, waliopanga foleni kusubiri kuhudumiwa. Hilo halijawahi kutokea, hivyo achana nalo, kama ndiyo unaanza biashara au unapanga kuanza biashara. Hata kama watu wanakuahidi kiasi gani kwamba watanunua kwako, ukweli unaupata unapoanza biashara, hutawaona. (more…)

BIASHARA LEO; Kuwa Makini Unapoingia Kwenye Biashara Mpya, Hata Kama Umeshazoea Biashara…

By | July 26, 2017

Kila biashara ina changamoto zake, hii ina maana kwamba kama umekuwa kwenye biashara fulani kwa kipindi kirefu, na umeshajifunza na kuzoea biashara, haimaanishi unaweza kufanya kila aina ya biashara. Utakuwa na unafuu ukilinganisha na ambaye hajawahi kufanya biashara kabisa, lakini bado unahitaji kujifunza kwenye kila biashara mpya unayoingia. Watu wengi (more…)

BIASHARA LEO; Maana ya neno HAPANA kwenye biashara…

By | July 24, 2017

Kama unafanya biashara na hujawahi kuambiwa neno HAPANA, huenda kuna makosa unafanya kwenye biashara yako. Labda unaifanya kwa viwango vya chini sana, au huna mpango wa kuikuza. Lakini kwa kawaida, neno HAPANA utalisikia sana kwenye biashara, mno yaani. Na utalisikia kwa kila mtu, kuanzia wateja wako, wafanyabiashara wengine, washirika wako, (more…)

BIASHARA LEO; Teknolojia Pekee Mteja Anayojali Kwenye Biashara Yako Ni Hii.

By | July 23, 2017

Kila ninapokuwa nawauliza watu nini kinawazuia kuingia kwenye biashara, majibu huwa yananishangaza mno. Watu huwa wanataja vitu ambavyo unashangaa vinawezaje kumzuia mtu asiingie kwenye biashara anayotaka kuingia. Watu wengi wamekuwa wakisubiri mpaka wawe kamili kwa kila kitu, mpaka waandae na vipeperushi vya kuwavutia wateja ndiyo waanze biashara rasmi. Lakini unajua (more…)

BIASHARA LEO; Ipe Biashara Muda, Usikimbilie Hatua Kubwa Haraka…

By | July 22, 2017

Kwa muda wote ambao nimekuwa najifunza biashara, kupitia mafunzo mbalimbali na hata kufanya biashara, nimekuwa nafananisha biashara na kitu kimoja muhimu; maisha ya mwanadamu. Nashawishika, bila ya shaka yoyote kwamba biashara ina sifa kama ya mwanadamu, kabisa. Biashara zinazaliwa, biashara zinakua, na biashara zinakufa, kama ilivyo kwa binadamu. Ili biashara (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujafanya Maamuzi Kutokana Na Maoni Ya Watu, Fikiria Hili…

By | July 21, 2017

Unapofanya biashara, hasa kwa mazingira yetu ambayo kila mtu ni mshauri wa biashara, utapata maoni mengi sana kutoka kwa kila mtu. Hata mtoto wa shule ya msingi anaweza kukushauri ni namna gani bora ya kufanya biashara yako. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanakimbilia kufanya maamuzi makubwa ya biashara zao kwa sababu ya (more…)

BIASHARA LEO; Jifunze Kwenye Kila Aina Ya Biashara…

By | July 20, 2017

Moja ya kosa kubwa ambalo wafanyabiashara wengi huwa wanafanya, ni kutokujifunza kupitia biashara nyingine. Na hata kama wakijifunza, basi hujifunza kwenye biashara zinazofanana na zile ambazo tayari wanazifanya. Kwa njia hii huwa hawaji na kitu kipya, badala yake kuiga kile ambacho tayari wengine wanafanya. Njia bora kabisa ya kujifunza kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Faida Siyo Kusudi La Biashara…

By | July 19, 2017

Kuna watu huwa wanaingia kwenye biashara kwa kusudi la kutengeneza faida, kupata fedha za kuendesha maisha yao, ni kitu kizuri, maisha lazima yaende na fedha ni muhimu. Lakini umuhimu wake unaenda mpaka pale mtu anapoondoka kwenye hofu ya kukosa fedha, na hapo ndipo mtu anaona kuna kitu anakosa kwenye maisha (more…)

BIASHARA LEO; Epuka Kosa Hili La Muda Unapoanza Biashara Yako.

By | July 18, 2017

Kuna kosa moja kubwa sana la muda ambalo watu wengi wanaoingia kwenye biashara huwa wanalifanya. Kosa hilo ni kujikadiria muda mdogo wa biashara kuweza kusimama yenyewe na kupata faida. Watu wengi huingia kwenye biashara wakitegemea kuanza kutengeneza faida ndani ya muda mfupi tangu wanapingia. Lakini uhalisia umekuwa ni tofauti na (more…)

BIASHARA LEO; Changamoto kubwa kwenye kupata wateja…

By | July 17, 2017

Zipo changamoto nyingi za biashara, na kwenye kupata wateja zipo changamoto pia. Lakini ipo changamoto moja kubwa ambayo wafanyabiashara wengi, huwa hawaielewi. Hasa kwa wale wafanyabiashara wanaoanza, huwa hawaelewi changamoto hii kwa sababu bado wanakuwa hawajawaua wateja wa biashara zao. Changamoto tunayokwenda kuigusia leo ni kuchagua wateja wa biashara yako. (more…)