Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Usikimbilie Kufanya Vitu Rahisi, Vitakupoteza Kibiashara…

By | June 28, 2017

Biashara ni ngumu, hilo halina ubishi, lakini ugumu mwingine tumekuwa tunautengeneza sisi wenyewe. Hasa pale ambapo tunakuwa tunatafuta njia rahisi ya kufanikiwa kwenye biashara. Kwa kuwa kufikiri ni kazi ngumu, na kwa kuwa njia bora za kuifanikisha biashara yako kutakuhitaji ufikiri, watu wanakwepa hilo. Na badala yake wanaangalia kipi rahisi (more…)

BIASHARA LEO; Tengeneza Utegemezi Wa Mteja Kwenye Biashara Yako….

By | June 27, 2017

Mahusiano yoyote bora na ya aina yoyote ile, yamejengwa kwenye msingi wa utegemezi. Pale ambapo kila mmoja anamtegemea mwenzake kwa kitu fulani, ndipo umuhimu wa kila mmoja unapoonekana na mahusiano kuwa bora, pale ambapo kila mtu anatimiza kile anachotegemewa. Kwenye biashara pia hali ni hiyo, pale mteja na mfanyabiashara wanapokuwa (more…)

BIASHARA LEO; Kama Fursa Inaongelewa Na Kila Mtu, Umeshachelewa…

By | June 26, 2017

Makosa ya binadamu ni yale yale, miaka nenda miaka rudi. Mwaka 2000 palitokea mgogoro wa kiuchumi, hasa nchini marekani, ambapo hisa za makampuni ya mtandao wa intaneti zilishuka ghafla. Hali hii ilipelekea wengi ambao walikuwa wanaonekana mamilionea, kufilisika kabisa. Kilichopelekea hali hii ni kuvuma kwa habari za biashara ya intaneti, (more…)

BIASHARA LEO; Je kinafanya kazi?

By | June 25, 2017

Unapokuwa mfanyabiashara, maisha yako unayajenga kwenye msingi wa kuuza vitu, yaani unapata kipato cha kuendesha maisha, kupitia kile unachouza. Sasa kwa kuwa hayo ni maisha, lazima uwe makini sana kwa sababu kosa dogo unaloweza kufanya, litakuwa na madhara makubwa sana kwako. Wapo watu ambao wameharibu biashara zao kwa makosa madogo (more…)

BIASHARA LEO; Kamwe Usimlalamikie Mteja….

By | June 24, 2017

Ndiyo kuna wateja wasumbufu, wateja ambao wanayafanya maisha yako kibiashara kuwa magumu mno. Wateja wanaotaka kunufaika wao bila ya kujali biashara yako. Wateja wanaotaka kupata zaidi kwa kutoa kidogo. Wateja wanaokopa na hawalipi. Wateja ambao wakishakopa wanahama kabisa. Lakini nisichotaka wewe ufanye ni kukaa na kuanza kuwalalamikia wateja wa aina (more…)

BIASHARA LEO; Kikwazo Cha Elimu Kubwa Kwenye Mafanikio Ya Biashara….

By | June 23, 2017

Watu wengi wenye elimu kubwa wamekuwa wakishindwa kwenye biashara, huku wenye elimu za kawaida au za chini kabisa wakifanikiwa sana kwenye biashara. Hii ni kwa sababu, kufanikiwa kwenye biashara, haihitaji akili nyingi, na wakati mwingine akili nyingi zinakuwa kikwazo. Watu wenye elimu kubwa wamekuwa wakifikiria na kuchambua sana mambo, kiasi (more…)

BIASHARA LEO; Neno Lako Na Liwe Sheria….

By | June 21, 2017

Nilikuwa nasoma kitabu cha mfanyabiashara aliyeweza kufanya makubwa sana, alirithi biashara ya baba yake ya kuuza mvinyo, na akaweza kuikuza mara dufu ndani ya muda mfupi. Kwenye kitabu hicho alikuwa anasema ushauri bora kabisa wa biashara ambao baba yake alimpa ni huu; NENO LAKO LIWE SHERIA AMBAYO HUTAIVUNJA. Anasema baba (more…)

BIASHARA LEO; Kama Una Bango La Aina Hii Kwenye Biashara Yako, Liondoe Leo.

By | June 20, 2017

Biashara za karne hii ya 21 zimebadilika sana, lakini bado watu wengi wanafanya biashara zao kama vile tupo kwenye karne ya 19. Watu wanafanya biashara zao kwa mazoea na hili linawagharimu sana. Kuna bango moja huwa nashangaa kuliona mpaka leo kwenye maeneo ya biashara, au hata kwenye risiti za baadhi (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Yako Ni Kuwafurahisha Watu…

By | June 19, 2017

Hitaji kubwa sana la kila mwanadamu, ukishaondoa yale ya kuhakikisha anaendelea kuwa hai, basi ni kujaliwa na wengine, kuonekana wa thamani mbele ya wengine. Hichi ni kitu ambacho watu wanakipigania kweli. Yaani ukiwaangalia watu usoni ni kama wamejibandika ujumbe unaosema TAFADHALI NITHAMINI…. Watu wanapenda sana hilo. Watu wanapothaminiwa, wanapoona wana (more…)