Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Anza Kuiua Biashara Yako Wewe Mwenyewe….

By | June 18, 2017

Ukweli ni kwamba, watu wamekuwa wanaua biashara zao wao wenyewe, bila ya kujua kama wanafanya hivyo. Na hili linakuwa changamoto kwao kwa sababu wanakuja kustuka mambo yakiwa yameshaharibika sana. Wateja wameshaondoka, hasara imeshakuwa kubwa na hakuna namna ya kuiokoa tena biashara ile. Mimi ninachotaka kukuambia leo ni uanze kuiua biashara (more…)

BIASHARA LEO; Urahisi Wa Biashara Na Thamani Ya Biashara…

By | June 17, 2017

Biashara rahisi kufanya, thamani yake ni ndogo, na biashara ngumu kufanya, thamani yake ni kubwa. Kwa maneno mengine, biashara rahisi kufanya faida yake ni kidogo, na biashara ngumu kufanya faida yake ni kubwa. Watu wengi wamekuwa wakikimbilia kutafuta biashara rahisi kufanya, biashara ambayo haitawapa stress, biashara ambayo wana uhakika wa (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Viwili Vinavyojenga Biashara Yenye Mafanikio.

By | June 16, 2017

Biashara zote zenye mafanikio, zinajengwa kwenye vitu viwili vikuu; Bidhaa au huduma nzuri. Wateja wanaojirudia. Unahitaji kuwa na bidhaa au huduma nzuri, siyo nzuri kwa sura, bali nzuri kwa uhitaji wa watu. Kile unachouza lazima kiwe kinatatua tatizo au kutimiza mahitaji ya wateja wako. Kiwe na thamani kwao inayowafanya kuwa (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Mtarajiwa…

By | June 2, 2017

Biashara yako ina wateja ambao ni wale watu wanaonunua kwako sasa. Hawa tayari wanakujua na wanajua ni kipi unachotoa na kinawasaidiaje. Lakini pia biashara yako ina wateja watarajiwa. Hawa ni wale watu ambao bidhaa au huduma unayotoa inawafaa na itawasaidia, ila bado hawajawa wateja wako bado. Zipo sababu nyingi zinazoweza (more…)

BIASHARA LEO; Fukuza Wateja Hawa…

By | August 31, 2016

Nimekuwa nakuandikia na kukushauri kuhusu biashara kwa muda sasa, nafikiri unashangaa ninapokuambia ufukuze wateja. Kabla hujashangaa, soma kwa makini ili mwisho uweze kufanya maamuzi sahihi ya biashara yako. Tatizo la wafanyabiashara wengi. Wafanyabiashara wengi wamekuwa na tatizo moja, ambalo limekuwa linawasumbua sana na kuwazuia kukuza biashara zao. Tatizo hilo ni (more…)

BIASHARA LEO; Cross-Selling Na Up-Selling, Mbinu Mbili Za Kuongeza Mauzo Bila Kuongeza Wateja.

By | August 29, 2016

Linapokuja swala la kuongeza mauzo ili kuongeza faida kwenye biashara, wafanyabiashara wengi huwa wanaangalia sehemu moja pekee, kuongeza wateja wengi zaidi. Kuongeza wateja ni mbinu muhimu ya kibiashara kwa sababu biashara yako inaweza kuwafikia watu wengi zaidi. Na kadiri unavyokuwa na wateja wengi, ndivyo unavyotengeneza uhuru wa biashara yako. Lakini (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Kitakachotokea Kwenye Biashara Yako Mpaka Ufanye Vitu Hivi Viwili…

By | August 3, 2016

Hakuna kitakachotokea kwenye biashara yako mpaka pale utakapofanya vitu hivi viwili muhimu sana na kwa mfuatano sahihi. Kwanza muuzie mtu kile unachotoa, iwe ni huduma au bidhaa. Pili mtu aridhishwe na kile ulichomuuzia. Hii ndiyo misingi inayobeba biashara yako. Mengine yote unayofanya kwenye biashara kama hayaipeleki biashara kwenye misingi hii (more…)

BIASHARA LEO; Kuwa Sehemu Sahihi Kwa Wakati Sahihi…

By | July 29, 2016

Moja ya vitu ambavyo unahitaji kwenye biashara ni kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi. Na taarifa hizi zitakuwezesha wewe kufanya maamuzi sahihi kwa pale ulipo kibiashara ili kuweza kusonga mbele zaidi. Mafanikio ya biashara yanategemea wakati uliopo na kile unachofanya. Kwa mfano mtu aliyekuwa anajua matumizi ya kompyuta wakati (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kuifanya Biashara Yako Kuwa BRAND.

By | July 28, 2016

Brand ni lile jina ambalo biashara inakuwa imejijengea kwenye jamii na wateja wake. Ni ile sifa ya kipekee ambayo biashara inayo na inajulikana na wengine. Coca Cola ni brand, unaposikia tu neno coca cola unajua ni kinywaji bora, hata kama hujawahi kunywa. Samsung ni brand, unaposikia neno samsung unajua ni (more…)

BIASHARA LEO; Ajiri Taratibu, Fukuza Haraka…

By | July 22, 2016

Mafanikio ya biashara yoyote yanatokana na falsafa ambayo biashara hiyo inaendeshwa nayo. Ukiangalia wafanyabiashara wengi wanaotokea kwenye nchi ambazo ni za kibepari, wana falsafa tofauti kabisa na wale wanaotokea kwenye nchi za kijamaa. Nchi za kibepari kama marekani, zina ushindani mkubwa sana wa kibiashara na hivyo watu kujali ubora wa (more…)