Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Kwa Mabadiliko Yanayoendelea Nchini, Ni Lazima Tubadili Mbinu Zetu Za Kibiashara Kama Tunataka Kufanikiwa.

By | July 21, 2016

Kumekuwa na kilio na malalamiko ya wafanyabiashara nchi nzima juu ya hali ngumu ya ufanyaji wa biashara. Tangu kumetokea mabadiliko ya uongozi kwenye nchi yetu Tanzania, kumekuwa na mabadiliko mengi yanayoendelea nchini. Mabadiliko haya yamebadili sana hali ya uchumi na hivyo kuvuruga mambo mengi ya kibiashara. Tunashuhudia biashara kubwa zikifungwa (more…)

BIASHARA LEO; Fursa Ipo Ndani Yako, Na Jinsi Ya Kuitumia.

By | May 4, 2016

Dunia imekuwa inatudanganya kitu kimoja, ya kwamba fursa zipo nje yetu na hivyo ni sisi kuhakikisha tunazitafuta na kuzitumia. Ukweli ni kwamba fursa hazipo nje yetu bali zipo ndani yetu. Tunapozijua fursa zilizopo ndani yetu,mkitu chochote kinachotuzunguka kinakuwa fursa kubwa kwetu. Tutaweza kukitumia na kuweza kufanya mambo makubwa. Lakini kama (more…)

BIASHARA LEO; Mada Tatu Za Kuepuka Kwenye Mazungumzo Yako Ya Kibiashara.

By | April 28, 2016

Wewe kama mfanyabiashara, mara kwa mara utajikuta kwenye mazungumzo na watu wengine, ambayo yanahusu biashara au mambo mengine. Watu hawa wanaweza kuwa wafanyabiashara wenzako,  wateja wako au wawekezaji. Na mnaweza kuwa mmekutana kwenye mkutano au kwenye eneo la biashara. Katika kuzungumza, mada nyingi zinaweza kujitokeza na mkachangia. Hii ni vizuri (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kuwafikia Wateja Wengi Zaidi.

By | April 26, 2016

Ukuaji wa biashara yako unategemea idadi ya wateja unaowafikia. Kadiri unavyowafikia watu wengi zaidi wenye uhitaji wa kile unachotoa, ndivyo inavyokuweka kwenye nafasi kubwa ya kufanya nao biashara. Sasa hapa kuna maswali muhimu unayotakiwa kujiuliza ili uweze kuikuza biashara yako. Swali la kwanza; kama umeweza kutengeneza faida kwenye eneo la (more…)

BIASHARA LEO; Asichotaka Mteja Kusikia Kuhusu Biashara Yako.

By | April 22, 2016

Siku za nyuma biashara zilikuwa zinatangazwa kwa sifa za biashara hizo, lakini sasa hivi mambo yamebadilika, badala ya kutangaza biashara kwa ubora wake, sasa hivi biashara zinatangazwa kwa kile zinachofanya. Mteja hataki kusikia biashara yako inatumia teknolojia gani ya tofauti, mteja hataki kusikia biashara yako imemshinda nani na nani. Anachotaka (more…)

BIASHARA LEO; Ni Kiasi Gani Cha Faida Unawekeza Kwenye Biashara Yako?

By | April 19, 2016

Moja ya sababu kubwa kwa nini biashara nyingi huwa zinadumaa ni kukosekana kwa uwekezaji endelevu. Mtu anaanza biashara na miaka inapita lakini biashara inabaki pale pale, haikui wala kutanuka. Hii inasababishwa na mfanyabiashara kutumia faida yote anayoipata kutoka kwenye biashara yake. Kama na wewe unaendesha biashara yako kwa mtindo huu (more…)

BIASHARA LEO; Kushinda Mara Zote ni Kubaya Kibiashara.

By | April 15, 2016

Biashara inahitaji akili sana, biashara inahitaji kujua jinsi ya kwenda na akili na hisia za wengine. Na mambo mengi kwenye biashara hutafundishwa darasani wala kwenye mafunzo mengine ya kibiashara, bali utayaona mwenyewe kama utakuwa makini na biashara yako. Kwa mfano inapotokea wateja wanafanya makosa, na ikawa kweli ni makosa ya (more…)

BIASHARA LEO; Kuanzisha Biashara Ni Rahisi, Ugumu Uko Hapa…

By | April 13, 2016

Kuanzisha biashara ni rahisi, rahisi mno, unaweza kuanza biashara hata leo hii. Lakini kuanza biashara ambayo itakuwa endelevu na yenye mafanikio makubwa ni kazi ngumu sana. Ni ngumu kwa sababu kuna changamoto nyingi sana kwenye uendeshaji wa biashara yoyote ile. Na ugumu unaendelea kuwepo hata kama utakuwa na mtaji mkubwa (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Ya Mteja Kununua Unachouza, Anakununua Wewe Kwanza.

By | April 12, 2016

Biashara inaonekana rahisi pale unapofikiria kununua na kuuza pekee. Au kuandaa bidhaa au huduma yako kisha kusubiri wateja waje wa nunue. Lakini biashara siyo rahisi hivi, na ndio maana wengi wanashindwa. Kwa sababu huwa wanafikiri ukishakuwa na mtaji tu unaendesha biashara. Kinachoongeza ugumu kwenye biashara ni ile hali kwamba wateja (more…)

BIASHARA LEO; Makadirio Ya Matumizi Na Faida.

By | April 7, 2016

Unapoweka mipango yako ya kibiashara, ni lazima uwe na makadirio. Na linapokuja swala la fedha kuna makadirio mengi ambayo huwa tunayafanya kama wafanyabiashara. Tunakadiria matumizi yetu ya kibiashara, na pia tunakadiria mapato yetu na faida pia. Kitu kimoja cha kushangaza sana kuhusu makadirio yetu ni kwamba huwa siyo sahihi, karibu (more…)