Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Usitumie Biashara Mpya Kuua Biashara Yako Ya Zamani.

By | April 5, 2016

Unapoanza na biashara moja na ukaona inafanya vizuri, unapata mawazo ya kukua zaidi kibiashara, na kufikiria kufungua biashara nyingine mpya. Hili ni wazo zuri sana kwa sababu huwezi kubaki pale pale kwa siku zote, kama mfanyabiashara makini ni lazima ukue. Lakini hapa kwenye ukuaji, hasa wa kuanzisha biashara mpya kuna (more…)

BIASHARA LEO; Unachojifunza Kutoka Biashara Za Wengine.

By | April 1, 2016

Pamoja na kwamba wewe ni mfanyabiashara, bado pia wewe ni mteja kwenye biashara za wengine. Ukianzia na unapopata mahitaji yako muhimu na hata unapopata huduma nyingine muhimu kwako. Usiishie tu kuwa mteja, bali hakikisha kupitia uteja wako unajifunza mbinu za kuboresha biashara yako. Kila unapokwenda kununua kwenye biashara nyingine, jiulize (more…)

BIASHARA LEO; Njia Rahisi Ya Kuua Biashara Yako.

By | March 30, 2016

Kuna njia nyingi sana unazoweza kutumia kuua biashara yako. Kwanza elewa kwamba wewe mwenyewe ndiye utakayeua biashara yako. Siyo mtu mwingine yeyote, ni wewe kwa kufanya au kutokufanya mambo fulani kwenye biashara yako. Sasa turudi kwenye hiki tulichopanga kujadili leo. Njia rahisi sana ya kuua biashara yako ni kuacha kujali (more…)

BIASHARA LEO; Viashiria Kwamba Umeshaingia Kwenye Ushindani Utakaokupoteza Kibiashara.

By | March 25, 2016

Kama ambavyo nimekuwa nasisitiza mara nyingi, ushindani wa moja kwa moja kwenye biashara, ndiyo mchezo mbaya kuliko yote unaoweza kufanya kwenye biashara yako, kwa sababu utakupoteza haraka sana. Mfanyabiashara mwenzetu aliandika maoni kutaka kujua ni viashiria gani mfanyabiashara anaweza kuwa navyo pale anapokuwa ameingia kwenye mashindano ya kibiashara.Aliandika maoni yake (more…)

BIASHARA LEO; Kitu Kimoja Unachoweza Kumpoteza Nacho Mshindani Wako Wa Biashara.

By | March 23, 2016

Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara nyingi, kwenye biashara usiingie kwenye mashindano ya moja kwa moja na washindani wako, maana hii itakuumiza zaidi ya kukujenga. Unapoingia kwenye mashindano ya moja kwa moja, mshindani wako anaweza kufanya jambo lolote ambalo linaweza kuwaathiri wote wawili kwenye biashara zenu. Lakini pia nimekuwa nakushirikisha mbinu (more…)

BIASHARA LEO; Tofauti Ya Kutangaza Biashara Yako Na Kupiga Kelele.

By | March 17, 2016

Watu wengi wanaofikiri wanatangaza biashara zao, ukweli ni kwamba wanapiga kelele. Kabla hatujaendelea ni vyema tukajua kelele ni nini, ili tuone unahusianaje na wale wanaotangaza biashara. Kelele ni sauti zisizo na mpangilio au sauti zisizohitajika kwa mahali husika au wakati husika. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiwapigia watu wengi kelele kuhusu biashara (more…)

BIASHARA LEO; Sababu Ya Mteja Wako Kwenda Kwa Mshindani Wako.

By | March 16, 2016

Njia bora sana ya kuifikiria biashara yako, ni wewe mmiliki wa biashara kuvaa viatu vya mteja wako. Hebu fikiria kama wewe ndiyo ungekuwa mteja wa biashara hiyo unayoifanya wewe, je ungeendelea kuwa mteja wa biashara hiyo? Na unapofanya hivi usijaribu kujidanganya, ondoa hisia za kujipendelea na fikiri kwa kina. Kwa (more…)

BIASHARA LEO; Majukumu Makubwa Matano Kwa Kila Mmiliki Wa Biashara Kuzingatia.

By | March 15, 2016

Watu wengi hufikiri biashara ni kwenda kununua vitu kwa bei ya jumla, kuja kuviweka kwenye eneo lako la biashara na kuuza kwa reja reja. Unakaa eneo lako la biashara na mtaja akipita anaona upo pale unauza, anakuja, anauliza bei unamjibu, akitaka kununua unampa, kama asipotaka anaondoka. Au wengine wanafikiri ukishakuwa (more…)

BIASHARA LEO; Pumua Biashara Yako…

By | March 10, 2016

Mafanikio kwenye biashara siyo kitu rahisi, ila yanawezekana kama kweli ukijitoa. Na ninaposema kujitoa namaanisha kujitoa kweli kwenye kuifanya biashara yako. Leo nataka kukuambia, pumua biashara yako. Kwa nini upumue biashara yako? Kwa sababu pumzi ndio kitu ambacho huwezi kutengana nacho hata kwa dakika ukabaki salama. Hivi ndivyo ilivyo kwa (more…)

BIASHARA LEO; Huduma Bora Unazohitaji Kutoa Kwa Wateja Wako.

By | March 9, 2016

Kama ambavyo tumekuwa tunajifunza mara kwa mara, kuna eneo moja muhimu sana unaloweza kulitumia vizuri sana kwenye ushindani wa biashara. Japo sijuambii ushindane, ila unapokuwa vizuri kwenye eneo hili hata wale wanaofanya biashara sawa na yako watakuona kwa mbali tu. Eneo hili ni kutoa huduma bora sana kwa wateja wako. (more…)