Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Mambo Ya Kuzingatia Unapojikuta Kwenye Ushindani Wa Bei.

By | March 8, 2016

Kama ambavyo tumewahi kujifunza, hakuna ushindani ambao ni mbaya kwenye biashara kama ushindani wa bei. Huu ni ushindani mbovu sana na mara nyingi huwa nauita mbio za kuzimu. Yaani kama mnashindana kwa vigezo vya bei, kwa kuwa mara nyingi mnashindana kushusha bei, basi mwisho wa siku wote mnaishia kuwa na (more…)

BIASHARA LEO: Neno Ambalo Ni Marufuku Kumwambia Mteja.

By | March 7, 2016

Wewe kama mfanyabiashara makini, hitaji la kwanza kabisa ni kuijua vizuri biashara yako, nje ndani. Ni lazima wewe uwe mtaalamu wa biashara yako, kwa kizungu tunasema uwe expert kwenye hiyo biashara unayofanya. Kwa maana hiyo unahitaji kujua mengi kuhusu biashara yako na wakati huo huo unahitaji kuwa wazi kujifunza kuhusu (more…)

BIASHARA LEO; Huhitaji Wazo Jipya Kabisa, Ila Pia Usiige Kila Kitu.

By | March 4, 2016

Bado kuna watu wengi sana ambao wanashindwa kuingia kwenye biashara kwa sababu bado hawajapata wazo bora na la kipekee kwao. Kama na wewe ni mmoja wa watu hawa naomba nikupe taarifa leo ya kwamba unajidanganya na unapoteza muda wako bure. Huhitaji kuwa na wazo jipya kabisa na la kipekee ndio (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Ni Unachofanya, Siyo Unachosema.

By | March 3, 2016

Watu wengi wamekuwa wakiahidi mambo mengi sana kwenye biashara zao. Kuna wale ambao wamekuwa wakiahidi kuingia kwenye biashara na siku zinakwenda ila hawaingii. Na kuna wale ambao wamekuwa wakiweka mipango mizuri na bora kwa biashara ila hawafikii utekelezaji wa mipango hiyo. Ukweli ni kwamba kuahidi au kupanga ni sehemu ndogo (more…)

BIASHARA LEO; Hatua Za Kuchukua Pale Mteja Anapotaka Bei Ya Chini Kuliko Kiwango Chako.

By | March 2, 2016

Kwenye makala iliyopita ya BISHARA LEO, tuliona ni muhimu sana kuepuka kuweka bei kubwa ili wateja watakapotaka kupunguziwa ndiyo unampunguzia kufikia bei ya kawaida. Tukaona ni muhimu uwe na bei moja ambayo haipungui na kila mteja ataambiwa bei hiyo. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile bonyeza maandishi haya kuisoma; (more…)

BIASHARA LEO; Jambo Muhimu Kuzingatia Kwenye Bei Ya Bidhaa Au Huduma Unazotoa.

By | March 1, 2016

Inapokuja kwenye swala la upangaji wa bei za bidhaa au huduma tunazotoa, wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifanya kwa mazoea. Kuna hali fulani imezoeleka kwamba mteja ataomba kupunguziwa bei na ili kuhakikisha anapata faida, mfanyabiashara anaanza kumtajia mteja bei kubwa ili wakipunguzana bei irudi kule kwa kawaida. Haya ni mazoea ambayo siyo (more…)

#BIASHARA LEO; Aina Mbili Za Kushindwa Kwenye Biashara, Na Iliyo Bora Kwako.

By | February 29, 2016

Kuna aina mbili za kushindwa kwenye biashara na katika aina hizo mbili kuna moja ambayo ni bora kwako na nyingine siyo bora. Aina ya kwanza ya kushindwa kwenye biashara ni kuanzisha biashara halafu biashara hiyo ikafa. Hapa unajipanga na unaingia kwenye biashara ukiwa na malengo na mipango mizuri ila biashara (more…)

BIASHARA LEO; Wewe Ndiye Unayeijua Biashara Yako Na Siyo Mteja, Timiza Wajibu Huu.

By | February 19, 2016

Kuna wakati ambapo wafanyabiashara huwa tunajisahau sana. Tunapitiwa kwa kufikiri kwa kuwa sisi tunaijua biashara yetu basi mteja naye anajua. Au tunafikiri kwa sababu tumeshaeleza kwa wateja basi ni jukumu la kila mteja kujua. Ni jukumu lako wewe kumweleza kila mteja kuhusu biashara yako, na sio wote watakaokuelewa. Hivyo kuwa (more…)

BIASHARA LEO; Usiwe Nafuu Kuliko Wote.

By | February 17, 2016

Linapokuja swala la kuongeza mauzo na kukuza biashara, wafanyabiashara wengi huangalia eneo moja rahisi, kupunguza bei, au kuuza bei rahisi kuliko wengine. Hii inaweza kuonekana kufanya kazi kwa muda lakini baadaye itakuumiza, hasa kama utakuwa ndio bei nafuu kuliko wengine wote. Kama lengo lako ni kutengeneza biashara itakayokua na kudumu (more…)

BIASHARA LEO; Mbinu Kumi Anazoweza Kutumia Mfanyabiashara Mchanga Kuongeza Mauzo.

By | February 16, 2016

Uhai wa biashara ni sawa na uhai wa binadamu. Ili mtu uendelee kuwa hai ni lazima mzunguko wa damu uwe sawa. Na ili biashara iendelee kuwa hai ni lazima mzunguko wa fedha uwe sawa. Mzunguko wa fedha ndiyo damu ya biashara yoyote ile. Mzunguko wa fedha kwenye biashara unaanzia kwenye (more…)