Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Usimpe Mteja Anachotaka, Mpe Hiki.

By | February 15, 2016

Kwanza kabisa, kabla hatujachanganyana, unapoanza biashara, anza na biashara ambayo wateja wako tayari kununua. Hivyo ni lazima ujue matatizo ambayo watu wanayo na uje na suluhisho. Sasa pamoja na kuwa na kitu ambacho watu wanataka, bado usimpe mteja kile ambacho anataka yeye, bali mpe kile ambacho ni bora zaidi. Mteja (more…)

#BIASHARA LEO; Viwango Vya Kuepuka Kwenye Biashara Yako.

By | February 12, 2016

Kwenye biashara yoyote unayofanya au unayoingia kufanya, kuna viwango ambavyo waliotangulia kufanya biashara hiyo walishaviweka. Kuna utaratibu fulani ambao karibu kila mtu anayefanya biashara ya aina hiyo huwa anaufuata. Lakini ukichunguza kwa makini, huoni maana au mantiki yoyote ya kufanya kitu hiko. Hivi ni viwango ambavyo unahitaji kuviepuka, hivi ni (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kukabiliana Na Anayekuiga Kwenye Biashara.

By | February 11, 2016

Moja ya vitu ambavyo huwa nawashauri watu kwenye biashara na hata maisha ya kawaida ni kutokushindana. Ndiyo sisi binadamu tunapenda ushindani, lakini kushindana kwenye kazi, biashara na hata maisha ya kawaida huwa sio kuzuri. Sasa kama umeamua kutokushindana lakini ukaanzisha biashara kwa ubunifu wako mwenyewe na ukashangaa baada ya biashara (more…)

BIASHARA LEO; Chagua Wateja Kabla Ya Kuanza Biashara.

By | February 8, 2016

Moja ya changamoto ambayo wafanyabiashara wapya wanakutana nayo pale wanapoingia kwenye biashara, ni kukazana kwa kila kitu na hatimaye kuanza biashara, halafu wanakuta kwamba biashara haina wateja. Hii ni hali ambayo inaumiza sana hasa pale ambapo umejipanga kwa muda mrefu kuingia kwenye biashara husika. Hata kama upo kwenye biashara na (more…)

BIASHARA LEO; Njia Bora Ya Kutatua Mgogoro Kati Yako Na Mteja Wako.

By | February 5, 2016

Karibu tena kwenye makala hizi za biashara leo ambapo tunapeana mbinu za kuboresha biashara zetu zaidi. Na leo tutaangalia njia bora ya kutatua mgogoro unaoweza kuibuka kati yako na mteja wako. Kama ambavyo tumeshaona kwenye makala zilizopita, mara zote mteja yupo sahihi, na kama kuna ushindani wowote kati yako na (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Njoo Na ‘Chenji’ Yako.

By | February 4, 2016

Utawasikia wafanyabiashara wengi wadogo wakilalamika kwamba biashara ni ngumu sana. Watakupa kila sababu kwa nini biashara zao hazisongi mbele. Na unaweza ukakubaliana nao kabisa. Ila sasa nenda kwenye biashara hiyo asubuhi, nenda na noti ya shilingi elfu kumi na unataka kitu cha shilingi mia tano. Unaweza hata ukatukanwa, mfanyabiashara atakushangaa (more…)

BIASHARA LEO; Hisia Zako Weka Mbali Na Biashara.

By | February 3, 2016

Sisi binadamu ni viumbe wa hisia, japo tunapenda kufikiri kwa mantiki, lakini bado maamuzi yetu mengi tunayafanya kwa hisia. Hisia ni nzuri sana katika kujenga mahusiano mazuri, lakini ni mbaya sana katika kufanya maamuzi. Mara nyingi maamuzi unayofanya kwa hisia huishia kuwa ni maamuzi mabaya na yanayokugharimu kwakiasi kikubwa, iwe (more…)

BIASHARA LEO; Mara Zote Mteja Yupo Sahihi.

By | February 2, 2016

Karibu kwenye kipengele hiki ambapo tunakumbushana mambo muhimu kuhusu maendeleo na mafanikio ya biashara zetu. Leo tutagusia na kukumbushana eneo hili muhimu sana la biashara yako ambalo ni wateja. Na kuna kitu kimoja muhimu sana unatakiwa kukumbuka mara zote, ya kwamba mteja yupo sahihi mara zote. Inapotokea hali yoyote ya (more…)

#BIASHARA LEO; Kipengele Cha Biashara Leo Kinarudi.

By | February 1, 2016

Habari za wakati huu mwanamafanikio? Napenda kutoa taarifa kwamba kipengele cha BIASHARA LEO ambacho kinatoa makala fupi kuhusu mambo ya biashara kinarudi tena. Baada ya muda wa kutokuwepo kwa kipengele hiki, sasa kinarudi tena hewani. Kila siku kutakuwa na makala fupi kuhusu biashara kupitia kipengele hiki. Katika makala hizi tutaangalizia (more…)