Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Mbinu Za Kumrudisha Mteja Anayetaka Kukukimbia.

By | December 8, 2015

Kwenye makala ya jana ya #BIASHARA_LEO tuliona kauli moja ambayo ukiisikia kwa mteja maana yake mteja huyo unampoteza. Kama hukusoma makala ile bonyeza maandishi haya kuisoma kwanza kabla hujaendelea. Kwenye makala hiyo tumekubaliana usikubali kupokea kauli hii ya mteja. Sasa leo tutaangalia ufanye nini pale mteja anapokupa kauli kwamba nikiwa (more…)

BIASHARA LEO; Ukisikia Kauli Hii Kutoka Kwa Mteja Jua Umeshampoteza.

By | December 7, 2015

Wewe kama mfanyabiashara ni lazima uweze kuwaelewa wateja kwa njia mbalimbali. Kuelewa kile wanachosema, na jinsi wanavyokisema ikiambatana na vitendo vinavyoendana na kile wanachofanya. Kuna baadhi ya kauli ukizisikia kutoka kwa wateja zinakupa moyo kwamba ni dalili nzuri, lakini ukweli ni kwamba kauli hizo zinaashiria umeshampoteza mteja. Kauli moja muhimu (more…)

BIASHARA LEO; Wauzie Wanaoijua Thamani Unayotoa.

By | August 21, 2015

Moja ya njia unazotumia kupoteza muda na rasilimali nyingine kwenye biashara yako, ni kujaribu kumuuzia kila mtu kile unachouza. Ni vigumu sana kila mtu kuona thamani ya ile biashara ambayo unafanya. Hivyo katika harakati zako za kutafuta wateja utakutana na watu wengi. Kuna ambao wataiona thamani na kuchukua hatua haraka, (more…)

BIASHARA LEO; Tafuta Mlango Wa Kutorokea Na Jua Wakati Wa Kutoroka.

By | July 24, 2015

Biashara unayofanya sasa, haitakuwa hivyo ilivyo kwa miaka kumi ijayo. Japo kipindi hiko kuna watu ambao bado watakuwa wanaifanya kama inavyofanywa sasa. Ila hawa ni wale ambao wanaendesha biashara za kawaida, zinazowaumiza vichwa na zisizo na faida kubwa. Wajanja wote kwenye biashara wajua mlango wa kutorokea na wakati wakutoroka. Bado (more…)

BIASHARA LEO; Je Biashara Yako Inaendana Na Wateja Wako?

By | July 10, 2015

Tulishasema kwamba jambo muhimu kabisa kwenye biashara ni kujua mteja wako ni nani. Kama upo kwenye biashara na humjui mteja wako basi hujui ni nini unafanya kwenye biashara yako. Na ninaposema kumjua simaanishi kumjua kwa jina, bali kujua sifa za mteja wako kuanzia umri, kipato, anakoishi na mengine kama hayo. (more…)

BIASHARA LEO; Hili ndio tatizo la kushindana kwa bei na linavyokumaliza.

By | July 9, 2015

Tatizo la kushindana kwa bei kwenye biashara ni kwamba linawamaliza wote mnaoshindana. Watu wengi huwa wanafikiri kwamba kwa kuweka bei ndogo basi ndio wanavutia wateja wengi. Hivyo wanaweka bei ndogo na mwanzoni wateja wanakuja kweli, baadae mshindani wako naye anashusha bei na wateja wanaenda kwake tena. Mnafanya mchezo huu kwa (more…)

BIASHARA LEO; Je Umemridhisha Mteja Wako Leo?

By | July 8, 2015

Kama jibu lako ni sina mteja basi jitathmini vizuri. Kwanza kabisa kila mmoja wetu ana mteja, kama wewe ni mtu mzima na unaishi basi una mteja au una wateja wengi sana. Wateja hawaishii kwa wafanyabiashara tu. Wateja wapo kwa kila mtu. Kama wewe ni mfanyabiashara, mteja wako au wateja wako (more…)

BIASHARA LEO; Sikiliza Hawa Watu Wanaokupa Mawazo Ya Biashara Kila Siku.

By | July 3, 2015

Nikimaliza kuandika hapa na mtu akasoma, bado ataniandikia kwamba anatafuta wazo la biashara. Yaani wazo la biashara limechukuliwa kama ni kitu kikubwa sana ambacho watu wanapigana nacho ili wakipate. Ni kama ukishapata wazo basi mambo yako yote yamenyooka. Nimekuwa nikisema mara kwa mara mwamba wazo la biashara linaanza na wewe (more…)

BIASHARA LEO; Hiki Ndio Kitu Pekee Kitakachoifanya Biashara Yako Ndogo Iweze Kumudu Ushindani.

By | July 1, 2015

Kama unaendesha biashara ndogo, au unaendesha biashara mpya ambayo tayari kuna watu wengine ambao wanaifanya biashara hii kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe, basi una njia nyembembe sana ya kuweza kufanikiwa. Ukweli ni kwamba hawa waliopo kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko (more…)

BIASHARA LEO; Mpango Wa Biashara Sio Biashara.

By | June 30, 2015

Nina mpango mzuri sana wa biashara, biashara hii itakuwa na wateja wengi na itatengeneza faida kubwa. Asante kwa mpango huo mzuri, lakini elewa kwamba mpango wa biashara sio biashara. Unaweza kuandika vizuri sana kwenye karatasi zako mteja wako ni nani, yupo wapi na utawezaje kumfikia, lakini hii sio biashara. Sisemi (more…)