Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Hapa Ndio Biashara Yako Inapokosa Maana…

By | May 25, 2015

Unapojaribu kuwa kila kitu kwa kila mtu biashara yako inakosa maana na unashindwa kuwa chochote kwa yeyote. Ufanye nini basi; kuna wa pekee kwa kundi fulani la watu. Usitake kumpata kila mteja aliyepo hapa duniani, bali lenga kuwapata wale watu ambao utaongeza maana kwenye maisha yao, utatatua matatizo yao na (more…)

BIASHARA LEO; Kama Bado Hujawa Tayari Kuingia Kwenye Biashara…

By | May 23, 2015

Watu wengi wamekuwa wakiniandikia kwamba wanataka kuanza biashara ila bado hawajawa tayari. Wanakuwa na sababu nyingi ambazo huzitumia na hufikiria wakimaliza mambo fulani kwanza ndio wataingia kwenye biashara. Sasa kama na wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kwamba bado hawajawa tayari kuingia kwenye biashara, nataka nikuambie kitu kimoja, hakuna (more…)

BIASHARA LEO; Tafuta Wenye Maumivu…

By | May 22, 2015

Unaweza kuw ana biashara nzuri sana, una bidhaa au huduma bora kabisa inayoweza kutatua matatizo ya mtu na kuboresha maisha yake. Ila kila unapomwambia mtu kuhusu biashara yako, au unapowatangazia watu ambao unaona wanafaa kuwa wateja wako, hawaonekani kuwa tayari kununua bidhaa au huduma hiyo. Katika hali kama hii ni (more…)

BIASHARA LEO; Sahau Kuhusu Kuongeza Faida Na Fanyia Kazi Kitu Hiki Kimoja Kwanza.

By | May 21, 2015

Lengo la biashara sio kutengeneza faida. Kama utakataa sentensi hiyo na una biashara fanya jaribio. Endesha biashara yako kwa lengo moja tu, kupata faida. Na hivyo tumia njia yoyote unayoona itakuwezesha kukuletea faida. Utaipata faida hii kwa muda mfupi lakini biashara haitokua, itakufa. Kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa makala (more…)

BIASHARA LEO; Kama Huwezi Kusema Kitu Hiki Kimoja, Huna Biashara.

By | May 20, 2015

Katika wakati wowote na popote ulipo ni lazima uweze kuielezea biashara unaofanya kwa sentensi moja. Ni lazima ndani ya dakika moja uweze kumweleza ni biashara ya aina gani unayofanya na inaelekea wapi, au ina mahitaji gani. Ukishindwa kufanya hivi basi hua biashara. Huna biashara kwa sababu huijui biashara yako vizuri (more…)

BIASHARA LEO; Kama Biashara Yako Isingekuwepo….

By | May 19, 2015

Leo kaa chini na ujiulize na kupata jibu la swali lifuatalo; Kama biashara yako isingekuwepo, je watu wanaokuzunguka wangekuwa katika hali gani? Je dunia ingekuwa kwenye hali gani? Kama jibu ni hakuna tofauti kati ya kuwepo au kutokuwepo kwa biashara yako, basi huna biashara, yaani upo tu unasukuma siku. SOMA; (more…)

BIASHARA LEO; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Kwenye Upangaji Wa Bei.

By | May 18, 2015

Kama kuna maji ya makampuni matatu sokoni na maji ya kampuni moja yakawa yanauzwa kwa bei rahisi kuliko ya makampuni mengine, wateja watanunua yapi? Haihitaji elimu kubwa kujua kwamba watanunua yale maji yanayouzwa kwa bei rahisi. Wateja wengi watanunua maji hayo. Hii ni kwa sababu maji hayatofautiani sana, maji ni (more…)

BIASHARA LEO; Kinachokufanya Ushindwe Kutekeleza Mipango Yako.

By | May 16, 2015

Kila mfanyabiashara anayo malengo na mipango yake kwenye biashara anayofanya. Lakini ni wachache sana ambao wanaweza kufikia mipango yako na kuvuna matunda mazuri. Wafanyabiashara wengi huwa na mipango mizuri ila unapofika wakati wa utekelezaji ndio ugumu unaopoonekana. Hapa ndipo mtu anaona kama haiwezekani na kuamua kurudi nyume na kuendele akufanya (more…)

BIASHARA LEO; Bila Kudhulumu Watu Huwezi Kufanikiwa Kwenye Biashara…. UONGO.

By | May 15, 2015

Changamoto nyingi sana tunazokutana nazo kwenye biashara zinaanza na sisi wenyewe. Yaani wewe mwenyewe ndio chanzo kikubwa cha matatizo unayokutana nayo kwenye biashara yako. Japo huwezi kukubali hili ila nasikitika kukutaarifu hivyo. Biashara zinaposhindwa watu wanakuwa na sababu nyingi sana, uchumi mbaya, wateja hakuna, washindani ni wengi na kila aina (more…)

BIASHARA LEO; Unawachukia Wateja Wasionunua Kwako?

By | May 14, 2015

Nakumbuka zamani kidogo, ulikuwa kama umezoea kununua vitu kwenye duka moja, na siku kitu ulichokuwa unataka hukukipata, ukaenda kwenye duka jingine ambapo mfanyabiashara anajua huwa unanunua wapi, angeweza kukataa kukuuzia. Anaweza kukuambia kwamba kila siku unapita pale na kwenda kununua kwingine kwa nini leo uende kununua kwake. Mwingine anaweza kukataa (more…)