Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Usianze Biashara Upya Kila Siku…

By | May 13, 2015

Moja ya changamoto zinazowasumbua watu wengi kwenye biashara ni kuanza upya biashara kila siku na kila mara. Hali hii imefanya biashara zionekane ni ngumu sana kuliko ugumu wenyewe. Mtu anaanzaje biashara upya kila siku? Sio kwamba mtu anafunga biashara yake na kuanza upya, ila uendeshaji wake wa biashara unakua ni (more…)

BIASHARA LEO; Upya Wa Biashara Mpya Na Unavyoweza Kuutumia Vizuri…

By | May 12, 2015

Biashara mpya zimekuwa na mambo mengi sana. Kuna biashara ambazo huwa zinaanza kwa wateja wachache sana na kuna nyingine zinaanza na wateja wengi sana. Biashara zinazoanza na wateja wachache tulishajadili hapa na hatua gani za kuchukua. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ile isome hapa; Aina Tatu Za Wateja Na (more…)

BIASHARA LEO; Njia Kumi Rahisi Za Kufukuza Wateja…

By | May 11, 2015

Mara nyingi huwa tunafanya mambo kwa mazoea. Na kutokana na mazoea hayo tunasahau kwamba matokeo ya kile tunachofanya yanaweza kuwa mabaya sana kwenye biashara zetu. Kuna njia uliyozoea kufanya biashara yako ambapo kwa njia hiyo unafukuza wateja wengi zaidi ya wale ambao unawakaribisha. Na hii imekuwa inaumiza biashara yako kidogo (more…)

BIASHARA LEO; Anza Na Tatizo Ulilonalo, Halafu Biashara.

By | May 9, 2015

Katika kila mazingira ambayo mtu yupo kuna fursa nyingi sana za biashara. Huhitaji kuwa na shahada ili kujua hili, ila bado limekuwa ndio swali ambalo linaulizwa sana. NIFANYE BIASHARA GANI? AMBAYO ITANILIPA? Sichoki kujibu swali hili kwa sababu kazi yangu mimi ni kukupa wewe maarifa yatakayokusaidia kukuza biashara yako na (more…)

BIASHARA LEO; Kuhusu Wateja Wasionunua Kwako.

By | May 8, 2015

Kwenye biashara unayofanya, kuna wateja ambao unajua kabisa wanaweza kunufaika na biashara yako, ila mpaka sasa hawanunui kwako. Je umewahi kujiuliza ni kwa nini? Kama bado unapoteza wateja wengi sana, hao unaowajua tayari na hata ambao bado hujawajua. Kwenye biashara, kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida, hakuna kitu kinachotokea kw (more…)

BIASHARA LEO; Tengeneza Mtandao Wako.

By | May 7, 2015

Kitakachokusaidia kufanikiwa kwenye jambo lolote sio kile ambacho unakijua bali wale ambao unawajua. Kadiri unavyojua watu wengi ndivyo unavyoongeza nafasi zako za kufanikiwa kwenye biashara yako. Ni muhimu sana kwako kukuza mtandao wako wa kibiashara. Hakikisha watu wengi unaowajua na hata usiowajua wanajua biashara yako. Hakikisha biashara yako unaweza kuieleza (more…)

BIASHARA LEO; Mlazimishe Farasi Kwenda Mtoni Na Mlazimishe Kunywa Maji.

By | May 6, 2015

Wahenga walisema kwamba unaweza kumlazimisha farasi kwenda mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Kwa upande wa biashara, kauli hii sio kweli hata kidogo. Kwenye biashara unaweza kumlazimisha farasi kwenda mtoni na pia ukamlazimisha kunywa maji. Na wala hutumii nguvu kubwa sana, yaani ukishamfikisha karibu na maji tu yeye mwenyewe akayakimbilia. (more…)

BIASHARA LEO; Kama Mteja Anaweza Kununua Kwa Mtu Yeyote, Kwa Nini Anunue Kwako?

By | May 5, 2015

Swali rahisi sana; kama mteja anaweza kununua kwa mtu yeyote, kwa nini aje kununua kwako? Unaweza kujibu swali hili? Kama huwezi upo kwneye hatari. Ila usijali, nipo hapa ili tuweze kusaidiana ili uweze kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Kama mteja anaweza kununua kw amtu yeyote na hana sababu nyingine yoyote (more…)

BIASHARA LEO; Huwezi Kuwa Sahihi Mara Ya Kwanza.

By | May 4, 2015

Kuna swali ambalo huwa linaulizwa tena na tena na tena yaani kila siku swali hili linaulizwa. Hata nitakapomaliza kuandika hapa, mtu akipiga simu au kuandika email atauliza swali hilo. Swali lenyewe ni NIFANYE BIASHARA GANI AMBAYO INA FAIDA SANA, au NI BIASHARA GANI AMBAYO INALIPA SANA KWA SASA. Na jibu (more…)

Hii Ni Nafasi Ya Mwisho Kabisa, Usiikose Tena.

By | May 2, 2015

Kwanza niwashukuru sana wale wote ambao wameshajiunga na semina ya MAFANIKIO KATIKA BIASHARA  mwaka 2015. Umefanya maamuzi sahihi sana kujiunga na semina hii na utajifunza mambo mazuri ambayo kama utayatumia utaboresha zaidi biashara yako na kufikia mafanikio makubwa. Nimepokea ujumbe kutoka kwa watu wengi jana kusumbuliwa na mtandao hivyo kushindwa (more…)