Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Maeneo Sita Unayopaswa Kuwa Sahihi Kwenye Biashara Yako.

By | July 21, 2018

Mafanikio kwenye biashara siyo kitu kigumu kama wengi wanavyofikiri. Ni kujua kanuni sahihi ya mafanikio ya biashara yako, kisha kuifanyia kazi huku ukiwa na subira na uvumilivu. Wengi wanaoshindwa kwenye biashara wanakosa kanuni sahihi ya kufanyia kazi au wanakosa subira na uvumilivu. Na kwa kuwa mafunzo ya biashara ni mengi, (more…)

BIASHARA LEO; Kila Unachofanya Kwenye Biashara Yako, Anza Na Mteja…

By | July 19, 2018

Kuna maamuzi mengi ambayo watu huwa wanafanya kwenye biashara zao. Lakini cha kushangaza maamuzi mengi yanayofanywa, ni kwa sababu ya mmiliki wa biashara na siyo kwa sababu ya mteja. Mtu anaamua kufanya kitu kwa sababu yeye ndiye anayependa kiwe hivyo, na siyo kwamba mteja ndiyo anapenda kiwe hivyo. Unapokuwa kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Machaguo Mawili…

By | July 18, 2018

Kikwazo namba moja kwenye mauzo katika biashara nyingi ni mteja kukosa machaguo zaidi wakati ananunua. Mteja anaweza kuja kwenye biashara yako, akiwa na shida au uhitaji fulani. Wewe kama mfanyabiashara ukamweleza na kumpa kile ambacho unaona kinamfaa. Sasa utafanya kosa kubwa sana, kama utampa kitu kimoja tu. Maana wakati wote (more…)

BIASHARA LEO; Kupunguza Bei Ni Uvivu Kibiashara…

By | July 17, 2018

Kama unapunguza bei kwa sababu gharama zako za uzalishaji au za kuendesha biashara zimepungua na unajali wateja wako wapate kilicho bora, hongera sana. Lakini kama unapunguza bei kwa sababu unataka wateja wengi zaidi waje kwako badala ya kwenda kwa washindani wako kibiashara, nina habari mbaya kwako, huo ni uvivu wa (more…)

BIASHARA LEO; Kwenye Biashara Ndogo, Mafanikio Yanategemea Kitu Hichi Kimoja…

By | July 16, 2018

Biashara ndogo ni biashara ngumu sana kufanya, kwa sababu wewe mfanyabiashara ndiyo unakuwa kila kitu kwenye biashara yako. Maamuzi yote kwenye biashara yako yanakutegemea wewe, na kwa wingi wa majukumu yako, ni rahisi kushindwa kuweka mkazo kwenye maeneo muhimu ya ukuaji wa biashara yako. Unapokuwa kwenye biashara ndogo, kila siku (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Hatakumbuka Zaidi Bei, Bali Hichi Muhimu…

By | July 15, 2018

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifikiri kwamba kikwazo cha wateja kununua kwao ni bei. Wengi wanashawishika kwamba wakishusha bei basi watapata wateja wengi. Na wakijaribu kufanya hivyo mwanzoni wanaweza kuona ongezeko la wateja, lakini mwisho wa siku hilo haliwasaidii kwenye ukuaji wa biashara zao. Hii ni kwa sababu moja, wateja makini wa (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Yako Inapaswa Kumpatia Mteja Fedha Zaidi…

By | July 14, 2018

Mtazamo ambao unao kwenye biashara unayofanya, ni moja ya vitu ambavyo vitaifanya biashara hiyo ifanikiwe sana au ishindwe kabisa. Hata kama utafanya kila kinachopaswa kufanya, kama mtazamo siyo sahihi, bado biashara haitapata matokeo makubwa. Mtazamo ambao mfanyabiashara anao huwa unakuwa kikwazo au kichocheo kikubwa kwa mafanikio ya biashara hiyo. Kuna (more…)

BIASHARA LEO; Wakati Sahihi Wa Kupunguza Gharama Kwenye Biashara Yako Ni Huu…

By | July 13, 2018

Faida ndiyo kitu kinachofanya biashara iendelee kuwepo. Kama biashara haitengenezi faida, haitachukua muda mrefu, itakupa. Pamoja na kuweka juhudi kubwa kwenye kuongeza mauzo na mapato, sehemu kubwa inayopunguza faida ya biashara ni gharama za kuendesha biashara hiyo. Gharama za kuendesha biashara zinapokuwa kubwa, faida inakuwa ndogo au hakuna kabisa. Hivyo (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Unachofanya Mara Moja Kikawa Na Manufaa Kwenye Biashara Yako…

By | July 12, 2018

Hakuna kitu chochote ambacho ukifanya mara moja kitakuwa na manufaa makubwa kwenye biashara yako, hakuna kabisa. Mteja akinunua mara moja kwenye biashara yako na asinunue tena ni hasara kwako, hakuna faida yoyote unayotengeneza kwa mteja kununua mara moja. Mteja akija kwako na akanunua kitu kimoja huwezi kutengeneza faida nzuri kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Ambavyo Havilipi Moja Kwa Moja Kwenye Biashara Yako.

By | February 26, 2018

Kuna tabia moja ya waajiriwa ambayo nimekuwa naona inawarudisha nyuma sana kwenye kupiga hatua kwenye kazi hiyo. Tabia hiyo ni kufanya yale ambayo wanalipwa tu. Kama mtu halipwi moja kwa moja kwa kufanya kitu, basi hakifanyi. Na utawasikia kabisa wakijiambia kwani nalipwa? Tabia hii nimekuwa naiona pia kwa wafanyabiashara ambao (more…)