Category Archives: BIASHARA NA UJASIRIAMALI

BIASHARA LEO; Kuuza Vitu Vya Kawaida Kwa Watu Wa Kawaida…

By | September 20, 2018

Kwenye maisha, kitu ambacho ni rahisi kufanya, pia ni rahisi kutokufanya. Pia kitu ambacho ni rahisi kufanya, huwa hakina thamani kubwa, huwa hakilipi kama mtu anavyoweza kuwa anataka. Hivyo kwa kifupi, tunaweza kusema kuchagua kufanya vitu rahisi, ni kujiweka kwenye mstari wa kushindwa. Njia rahisi ya kuingia kwenye biashara ni (more…)

BIASHARA LEO; Kujenga Imani Ya Wateja Kwenye Bei…

By | September 19, 2018

Wafanyabiashara ndiyo tunaoharibu biashara zetu wenyewe, kwa sababu tunashindwa kutengeneza uaminifu kwenye biashara zetu. Mtu akija kwenye biashara yako, atauliza punguzo la bei, kwa sababu anajua na wewe utakuwa umeweka bei ya juu ili ukiulizwa punguzo uuze kwa bei unayotaka kuuza. Sasa hii ni njia ya hovyo sana ya kuendesha (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kujitengenezea Upendeleo Kwenye Biashara Yako…

By | September 18, 2018

Umewahi kwenda kwenye biashara mbili ambazo zinafanana, ukakuta kwenye biashara moja watu wamejipanga mstari kusubiri huduma, wakati biashara nyingine haina mteja kabisa? Yaani watu wapo radhi kusubiri wapate huduma kwenye biashara wanayotaka, kuliko kwenda kupata huduma pengine ambapo wangeokoa muda zaidi. Waswahili watakuambia anayejaza wateja anatumia dawa, au ushirikina, au (more…)

BIASHARA LEO; Weka Mkazo Kwenye Vitu Visivyobadilika…

By | September 17, 2018

Wapo watu wengi wameingia kwenye biashara wakifikiri ni fursa bora kumbe ni kitu cha msimu, kitu ambacho kinapita. Wapo wengine ambao wamebadili sana biashara zao wakijua mambo yamebadilika kumbe ni msimu tu wa kupita. Kabla hujafanya maamuzi muhimu kwenye biashara yako, kwanza angalia kinachokusukuma kufanya maamuzi. Je ni kitu cha (more…)

BIASHARA LEO; Adhabu Ya Mteja Asiyenunua Kwako…

By | September 16, 2018

Najua hili limekuwa linatokea kwenye biashara yako mara nyingi. Kuna mteja ambaye amekuwa hanunui kwako, anakupita na kwenda kununua kwa muuzaji mwingine, japo na wewe unauza kile anachokwenda kununua kule. Sasa inatokea siku moja, mteja huyo anaenda kule anakoenda kununua, anakosa kitu hicho, halafu anarudi kwako. Unachukua hatua gani kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Kama utaacha kuuza leo…

By | September 14, 2018

Kama ikatokea umeacha kuuza leo, je kuna watu watakaokosa kile unachouza? Je wapo watu ambao maisha yao yatakwama kwa sababu ya wewe kuacha kuuza kile unachouza? Kama ikitokea leo umeondoka kabisa kwenye biashara unayofanya, je kuna watu ambao watagundua uwepo wako? Iwapo ukiondoka hakuna anayegundua hata kama haupo, basi jua (more…)

BIASHARA LEO; Kuwapa Wateja Uhakika Wa Kile Unachowauzia…

By | September 13, 2018

Mbinu zote za kuwashawishi wateja kununua zimeshatumiwa sana kiasi kwamba wateja hawajui waamini kipi kati ya vingi wanavyoambiwa na kila mfanyabiashara. Sifa zote za bidhaa au huduma ambazo watu wanauza zimeshaelezwa mpaka mteja anakuwa na wasiwasi kama kweli sifa zinazoelezwa zipo. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinamshawishi kila mteja na (more…)

BIASHARA LEO; Cha Kufanya Pale Wengine Wanapopunguza Bei…

By | September 12, 2018

Changamoto kubwa kwenye biashara ni pale ushindani unapowekwa kwenye bei. Pale wenzako wanapopunguza bei ili kupata wateja zaidi. Ni rahisi kukimbilia na wewe kupunguza bei, lakini hiyo siyo mbinu ambayo itakuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa sababu unapopunguza bei, unapunguza faida na kadiri faidia inavyokuwa ndogo ndivyo huduma unazotoa zinavyokuwa za (more…)

BIASHARA LEO; Mkumbuke Mteja Mmoja Leo…

By | September 11, 2018

Leo fanya zoezi hili rahisi sana kwenye biashara yako, Mkumbuke mteja mmoja ambaye amewahi kununua kwako siku za nyuma, lakini siku za karibuni hujamwona akinunua tena. Ingia kwenye mawasiliano ya wateja wako, na chukua mteja mmoja, au wachache ambao hujawaona wakinunua mara kwa mara kisha fanya nao mawasiliano. Na mawasiliano (more…)

BIASHARA LEO; Aina Ya Uchumi Tunaoishi Sasa…

By | September 10, 2018

Watu wengi hawajui zama zimebadilika sana, na siyo tu kwenye sayansi na teknolojia, bali pia kwenye mahusiano. Sasa hivi hatuishi tena kwenye uchumi wa ujamaa au ubepari, bali tunaishi kwenye uchumi wa kujuana na wa huduma. Tunaishi kwenye uchumi ambao watu wanaojuana wanajaliana. Watu wananunua kutoka kwa watu wanaowajua, kwa (more…)