Category Archives: BIASHARA NA UJASIRIAMALI

BIASHARA LEO; Hakuna Njia Moja Sahihi Ya Kufanya Biashara Yako…

By | August 30, 2018

Moja ya vitu vinavyoua biashara nyingi ni mazoea. Watu wanakuwa wameanza biashara na kugundua njia moja ya kufanya biashara zao ambayo inawapa manufaa na kutumia njia hiyo kwa mazoea bila ya kubadili au hata kuwa bora zaidi. Watu wengine wamekuwa wanashauriwa kwamba njia pekee ya kufanikiwa ni kufanya biashara fulani (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Unavyotafuta Kwenye Biashara Ambavyo Hutavipata…

By | August 29, 2018

Nimekuwa nasema hili na bado naona wengi hawalipati vizuri. Watu wengi wanaingia kwenye biashara kwa sababu ambazo siyo sahihi, na hilo linawaumiza sana. Watu wanakuwa na mategemeo fulani wanapoingia kwenye biashara, lakini wakiingia wanakutana na uhalisia tofauti ambao unawaumiza sana. Watu wanaingia kwenye biashara wakiamini watakuwa na uhuru na muda (more…)

BIASHARA LEO; Sehemu Tatu Pekee Za Kuweka Nguvu Zako Kibiashara…

By | August 28, 2018

Kuna vitu vingi sana ambavyo wafanyabiashara wengi huwa wanafanya. Lakini sehemu kubwa ya vitu hivyo ni kupoteza muda na nguvu pia. Unaweza kuwaona watu wapo ‘bize’ sana, wanakazana kufanya kila kitu, lakini ukifanya tathmini ya yale wanayofanya, unagundua kwamba hayakuwa na umuhimu mkubwa. Kitu chochote unachofanya kwenye biashara yako, lazima (more…)

BIASHARA LEO; Kumbuka Kuna Mtu Anaweza Kuwa Rahisi Zaidi Yako…

By | August 27, 2018

Wafanyabiashara wavivu na wasiotaka kuweka kazi, huwa wanatumia njia moja kwenye kushindana. Njia hiyo ni kushusha bei na kuuza kwa bei rahisi zaidi ya wengine. Ni njia ambayo kwa haraka inaweza kuongeza wateja na faida, lakini baadaye inakuwa mzingo mkubwa kwa mfanyabiashara. Hii ni kwa sababu, kila mtu anaweza kupunguza (more…)

BIASHARA LEO; Ugonjwa Wa Fursa Mpya Utaua Ndoto Zako Kibiashara…

By | August 26, 2018

Pata picha ya mkulima huyu, Ameambiwa akilima karanga zitamlipa sana, analima shamba na kupanda karanga, wakati karanga zinaanza kuchipua, anaambiwa kuna fursa mpya, kama atalima mahindi, basi atafanikiwa sana, anang’oa karanga na kupanda mahindi. Mahindi yanakua na kabla hayajafikia kuvunwa, anaambiwa fursa kubwa sasa hivi ni maharagwe, anang’oa mahindi hayo (more…)

BIASHARA LEO; Hatua Mbili Za Kishujaa Za Kuchukua Kwenye Biashara Yako.

By | August 25, 2018

Biashara haina tofauti sana na vita, kwa sababu kufanikiwa kwenye biashara kunakutaka uwe shujaa kama walivyo mashujaa wa vita. Biashara nyingi zinazoanzishwa huwa zinakufa kwa sababu wanaoanza biashara hizo wanakuwa hawajajiandaa kisaikolojia kupambana na changamoto mbalimbali za biashara. Wengi hufikiri biashara ni wazo na mtaji, vingine vitakwenda. Lakini biashara ni (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Sababu Za Kutosha Za Kununua Kwako, Na Sasa.

By | August 24, 2018

Unapochagua mteja wa biashara yako, na ukaona kabisa ana sifa zote za wateja wa biashara yako. Yaani ana uhitaji ambao biashara yako inaweza kumtimizia na pia anaweza kumudu gharama unayotoza. Kama mteja huyo hatanunua, basi kosa litakuwa lako na siyo la mteja. Mteja, hasa mpya, hatakuwa tayari kununua kwako mpaka (more…)

BIASHARA LEO; Siyo Idadi Ya Wateja, Bali Ubora Wa Huduma…

By | August 23, 2018

Kipimo cha wengi kwenye ukuaji wa biashara kimekuwa ni idadi ya wateja wanaokuja kwenye biashara hiyo. Hivyo mfanyabiashara anapoona wateja wanaokuja ni wengi, anaona biashara unakuwa na ina mafanikio makubwa. Na hili ndiyo linalopelekea wafanyabiashara wengi kushusha bei ya bidhaa au huduma zao, ili kuvutia wateja wengi zaidi. Kwa sababu (more…)

BIASHARA LEO; Jifunze Kupitia Biashara Kubwa Kuliko Yako…

By | August 22, 2018

Unapotaka kujifunza zaidi kuhusu biashara, unahitaji kuziangalia biashara ambazo ni kubwa kuliko biashara unayoendesha wewe. Hii ni kwa sababu biashara kubwa zina changamoto za tofauti na biashara ambazo siyo kubwa. Na makosa wanayofanya wafanyabiashara wengi wanaoanza na biashara ndogo, ni kuendelea kuziendesha vile vile hata baada ya biashara kuwa zimeshakua (more…)

BIASHARA LEO; Hatari Ya Biashara Yako Kufanikiwa…

By | August 21, 2018

Unapoanzia biashara yako chini kabisa, watu wengi hawakupi uzito. Watu wengi wanaona ni biashara ndogo, ambayo haiwezi kufanikiwa. Wapo mpaka watakaokukatisha tamaa na kukuambia huwezi. Sasa wewe unakomaa, una ndoto yako unayofanyia kazi na biashara inaanza kukua, biashara inaonesha mafanikio makubwa. Hapo sasa ndipo hatari ya biashara yako inapoanzia. Biashara (more…)