Category Archives: BIASHARA NA UJASIRIAMALI

BIASHARA LEO; Moja Kwa Ajili Ya Wote…

By | August 20, 2018

Kila mfanyabiashara huwa anapenda kuwa na wateja wengi awezavyo, kwa sababu ni kupitia wateja ndiyo biashara inatengeneza faida. Hivyo ndoto ya kila mfanyabiashara ni kuwa na wateja wengi zaidi, na wengi wanapoanzisha biashara, huwa wanalenga kumuuzia kila mtu. Hivyo hutawakuta wakiweka mipango ya kuwafikia wateja wa aina fulani, wao watakuwa (more…)

BIASHARA LEO; Usitawanye Nguvu Zako Kwa Yasiyo Muhimu…

By | August 19, 2018

Kuna watu wamekuwa wanaanzisha biashara, mwanzoni inaonekana kuwa na mafanikio makubwa, lakini haichukui muda inashindwa au hata kufa kabisa. Kinachotokea ni kwamba mtu anakuwa ameiona fursa, na anakuja na wazo la biashara ambalo linatoa suluhisho kwenye changamoto au uhitaji fulani. Basi wazo hilo linakuwa la kipekee na mafanikio yanaanza kuonekana. (more…)

BIASHARA LEO; Kisichoonekana Hakifikiriwi, Kisichofikiriwa Hakionekani…

By | August 18, 2018

Kwa kiingereza wanasema out of sight out of mind. Kama hukioni kitu, huwezi kukifikiria. Na pia kinyume chake itakuwa sahihi, kama hufikirii kitu, huwezi kukiona. Sasa utajiuliza kauli hii ina matumizi gani kwenye biashara yako. Na ukweli ni kwamba, kauli hii ina kila kitu kuhusu wateja wa biashara yako. Kuna (more…)

BIASHARA LEO; Usimsahau Mteja Huyu Wa Kwanza Na Muhimu Kwa Biashara Yako…

By | August 17, 2018

Mteja wa kwanza na muhimu sana kwa biashara yako, ni mtu yeyote ambaye anafanya kazi kwenye biashara yako. Wasaidizi wako kwenye biashara, yeyote yule anayejihusisha na biashara hiyo, ni mteja wa kwanza na wa muhimu sana kwenye biashara yako. Kwa sababu hawa ni wateja ambao wanaweza kuwakaribisha wateja wakanunua zaidi (more…)

BIASHARA LEO; Washauri Wako Kwenye Biashara…

By | August 16, 2018

Ni jambo la kushangaza lakini watu ambao hawajawahi kufanya biashara yoyote kwenye maisha yao wanaweza kugeuka kuwa washauri kwenye biashara yako. Wengi huamini kwa sababu wanaona biashara nyingi, basi wana mengi ya kushauri kwa biashara yoyote ile. Ni kweli kwamba kila mtu anaweza kuwa na ushauri mzuri kwenye aina yoyote (more…)

BIASHARA LEO; Njia Pekee Ya Biashara Ndogo Kuishinda Biashara Kubwa…

By | August 15, 2018

Watu wengi wanapokuwa na biashara ndogo zinazoshindana na biashara kubwa huwa wanajiona kama wapo upande wa kushindwa. Huwa wanaona biashara kubwa kwa sababu ina rasilimali nyingi basi itawashinda kwa urahisi sana. Lakini ipo njia ya biashara ndogo kuishinda biashara kubwa, ambayo wala haihitaji gharama za ziada. Njia hiyo ni kutengeneza (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Kitakachotokea Mpaka Umuuzie Mteja Kitu…

By | August 14, 2018

Uhai wa bishara yoyote unatoana na kitu kimoja, mauzo. Mauzo ndiyo njia pekee ya kuleta fedha kwenye biashara yako. Hivyo kwenye biashara yako, hakuna kitakachoweza kutokea mpaka pale mteja anapotoa fedha kununua unachouza. Hivyo nguvu zako zote unapaswa kuziweka kwenye kuhakikisha mteja anaelewa na kuwa tayari kununua. Lakini pamoja na (more…)

BIASHARA LEO; Usivunje Mioyo Ya Wateja Wako…

By | August 13, 2018

Tabia ya binadamu ni moja, tunapenda kuamini vitu na kisha kuvizoea. Kadiri vitu vinakwenda kama tulivyozoea viende, maisha yetu ni mazuri. Lakini vitu vinapokwenda tofauti na tulivyozoea, wakati tumeshaweka matumaini yetu kwenye vitu hivyo, hapo ndipo mgogoro unapoanzia. Hivi ndivyo unavyopaswa kwenda na wateja wako kwenye biashara yako. Wafanye wateja (more…)

BIASHARA LEO; Ushindani Utaondoa Faida Yote Na Kukuacha Huna Kitu…

By | August 12, 2018

Upo usemi maarufu kuhusu biashara kwamba biashara ni ushindani. Sasa kama utaubeba usemi huo na kuingia kwenye biashara kwa kuamini kwamba unaweza kushindana, unaweza ukashinda, lakini utabaki na ushindi usio na maana. Ushindi pekee unaohitaji kwenye biashara ni faida. Na faida ni pale gharama zako zote mpaka mteja anapata anachotaka, (more…)

BIASHARA LEO; Kitu Kimoja Kinachoweza Kuteketeza Biashara Yako Kabisa…

By | August 11, 2018

Watu wamekuwa wanatoa sababu mbalimbali kwa nini biashara zao zimeshindwa. Na unapowasikiliza, utawasikia wakisema mambo ya nje tu. Kwamba uchumi mgumu, kwamba watu hawana fedha, kwamba ushindani umekuwa mkali na mengine kama hayo. Hutawasikia wakisema mambo ya ndani, ambayo ndiyo sababu kuu ya kufa kwa biashara. Mambo kama uzembe, uvivu, (more…)