Category Archives: BIASHARA NA UJASIRIAMALI

BIASHARA LEO; Usijiachie Kwa Sababu Biashara Ni Yako…

By | August 10, 2018

Kitu kimoja nakiona kwenye biashara za wengi ni kwamba, wengi hawaheshimu biashara zao. Mtu anapokuwa ameajiriwa ataheshimu sana ajira yake. Atawahi kufika kazini na ataondoka pale muda wa kutoka unapofika. Hatajipangia tu safari zisizohusiana na kazi kama anavyotaka mwenyewe. Na hata jamii itamheshimu, haitamtegemea aamue tu chochote, kwa sababu kila (more…)

BIASHARA LEO; Njia Bora Ya Kufanikiwa Kwenye Biashara Ni Kuwa Na Ubinafsi Kwako Mwenyewe…

By | August 9, 2018

Kama unataka kuendesha biashara yako vizuri na kama unataka kufanya mambo mazuri kwenye hii dunia, basi jua ya kwamba unahitaji kujijali wewe kwanza kabla ya vitu vingine vyovyote. Ni kweli biashara itakuhitaji uweke juhudi kubwa, itahitaji muda wako mwingi, lakini kama hutajijali wewe mwenyewe kwanza, hutafika mbali. Utaweza kupata matokeo (more…)

BIASHARA LEO; Unatumia Mtego Gani Kuwanasa Wateja Wa Biashara Yako?

By | August 8, 2018

Kuwanasa wateja wa biashara yako ni hitaji muhimu sana kwa mafanikio ya biashara. Kwa sababu bila ya wateja kunasa, kuwa na kitu wanachokipata kwako tu, hawawezi kurudi tena kwako. Na kama ambavyo nimekuwa nakuambia, mteja akinunua mara moja kwako, ni hasara kwako. Unaanza kufaidika na mteja pale anaponunua tena na (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Wa Mfano Wa Biashara Yako…

By | August 7, 2018

Kosa moja wanalofanya wafanyabiashara wengi ni kuanzisha biashara zao kwa kujifikiria wao wenyewe, au kuangalia wafanyabiashara wengine wanafanya nini. Biashara yoyote inayoanzishwa na mtu kwa sababu anafikiria ananufaikaje na biashara hiyo pekee, au kwa kuwaangalia wengine wanaofanya biashara hiyo na kujiambia inalipa ndiyo maana wapo, lazima biashara hiyo ishindwe. Biashara (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujawauzia Wengine Bidhaa Au Huduma Yako, Wauzie Hichi Muhimu…

By | August 6, 2018

Umewahi kukutana na mtu ambaye anaweza kuuza kitu chochote kwa mtu yeyote. Yaani unaenda mahali, unajiambia kabisa kwamba hutanunua, lakini unakutana na mtu, na kwa jinsi anavyokupokea, kwa jinsi anavyokusikiliza, jinsi anavyokuelezea unachouliza, unajisikia vibaya kutokununua? Kama umewahi kuwa kwenye hali kama hiyo, basi unajua kwamba ulinunua kitu siyo kwa (more…)

BIASHARA LEO; Dawa Inayofanya Kazi Ni Inayouma…

By | August 5, 2018

Kuna tukio la kisaikolojia linatokea pale mteja anapotoa fedha yake aliyoipata kwa shida kukulipa kwa kile unachouza. Kwa sababu kwanza akishakupa fedha hiyo maana yake hawezi kuitumia kwa mambo mengine ambayo yanaweza kuwa muhimu kwake. Na pili, mteja anahitaji kupata uhakika kwamba anacholipia ni sahihi na moja ya kipimo anachotumia (more…)

BIASHARA LEO; Miliki Matatizo Ya Wateja Wako…

By | August 4, 2018

Kabla hujakimbilia kupunguza bei kwenye biashara yako kwa sababu wengine wanapunguza bei, kuna hatua nyingi unazoweza kuchukua na zikaongeza thamani sana kiasi kwamba bei yako inaonekana si kitu kulingana na mteja anachopata. Moja ya vitu unavyoweza kufanya ni kuyamiliki matatizo ya wateja wako. Yale matatizo ambayo biashara yako inatatua. Mfanye (more…)

BIASHARA LEO; Swali Moja Muhimu Kumuuliza Mteja Pale Anapokuambia Bei Yako Ni Kubwa Sana…

By | August 3, 2018

Usemi unaopaswa kuukumbuka kwenye biashara yako kila siku ni huu, mara zote mteja yupo sahihi. Hata kama kwa upande wako anakosea, jua kwamba kwa upande wake na kwa mtazamo wake, mteja mara zote yupo sahihi. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanafanya kosa sana kujaribu kuwaonesha wateja hawapo sahihi, kinachotokea wateja wanajisikia vibaya (more…)

BIASHARA LEO; Hamasa Yako Ni Muhimu Kuliko Unachouza…

By | August 2, 2018

Kosa moja ambalo wafanyabiashara wengi wanafanya pale wanapochagua biashara ya kufanya, ni kuangalia wafanyabiashara waliofanikiwa kwenye biashara fulani na kufikiri hiyo ndiyo biashara inayolipa. Lakini wanapoingia kwenye biashara hiyo, wanagundua siyo rahisi kama walivyoona kwa nje. Wanakutana na changamoto nyingi na hata wateja hawawi rahisi kuuziwa kama walivyofikiri. Rafiki, ukiona (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kujenga Himaya Yako Kibiashara…

By | August 1, 2018

Ili biashara ifanikiwe sana, lazima ijijenge kama himaya, imiliki sehemu kubwa ya soko, iwe na wateja wanaoitegemea biashara hiyo, wanaoiamini na ambao wapo tayari kuwaalika wengine kuja kwenye biashara hiyo. Hivyo badala ya kukazana kupata faida ya muda mfupi kwenye biashara yako, kazana kujenga himaya yako kibiashara, himaya ambayo itakuwa (more…)