Category Archives: FALSAFA MPYA YA MAISHA

Hapa unapata makala zinazokuwezesha wewe kujijengea falsafa mpya ya maisha yako. Ni kupitia falsafa yako ya maisha ndio unaweza kuwa na maisha bora yenye furaha na mafanikio.

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Jinsi Ya Kuishi Maisha Yenye Maana.

By | August 14, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye makala yetu ya leo ya falsafa mpya ya maisha, ambapo tunashirikishana maarifa muhimu ya kujenga maisha yenye furaha na mafanikio makubwa. Leo tutakwenda kuangalia kuhusu MAISHA YENYE MAANA, ikiwa ni swali ambalo nililizwa na mmoja wa rafiki na msomaji mwenzetu. Yeye alitaka kujua (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Jinsi Unavyoweza Kutumia Falsafa Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo.

By | August 7, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni imani yangu kwamba uko vizuri na maisha yako yanaendelea kuwa bora kila siku kupitia falsafa mpya ya maisha unayojijengea. Hatujifunzi tu falsafa hii mpya ya maisha ili tuwe tunajua sana, bali tunajifunza ili kuitumia kuboresha maisha yetu. Hivyo chochote unachojifunza, hakikisha unaweza kukitumia kwenye (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mbio Za Sakafuni, Zisizofika Ukingoni.

By | July 31, 2016

Mbio za sakafuni huishia ukingoni, huu ni usemi wa wahenga ambao una ukweli halisi. Kwa sababu kila sakafu ina ukingo, unapokimbia kwenye sakafu ukifika kwenye ukingo wa sakafu mbio zimeishia pale. Maisha yetu ni mbio za sakafuni, kwa sababu kila mmoja wetu anajua kwamba hatoishi milele, siku moja wote tutakufa, (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Hivi Ndivyo Unavyowapa Watu Wengine Ruhusa Ya Kukuumiza Wewe.

By | July 24, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Unayaonaje maisha yako kadiri unavyojijengea falsafa hii mpya ya maisha? Je unaona yanakuwa bora au yanazidi kuwa hovyo? Kwa sababu lengo kuu la falsafa hii mpya ya maisha ni kutuwezesha kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. Na kumbuka haya yote yanaanza na (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Sisi Ni Bora Kuliko Wao, Uongo Tunaojidanganya Mara Zote Na Kuharibu Mahusiano Yetu Ya Kijamii.

By | July 17, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni imani yangu kubwa kwamba unaendelea vyema huku ukiyaendesha maisha yako kwa misingi ya falsafa tunayojifunza kila siku. Maisha bora, yenye furaha na mafanikio yanaanza na wewe mwenyewe, kwa kuishi vile ambavyo unapenda kuishi, kwa kufanya kile ambacho unaweza kukifanya vizuri. Duniani tupo watu tofauti, (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; TATU MARA TATU, Vitu Vitatu Vyakufanya Kila Siku Ili Kuwa Na Maisha Bora Yenye Furaha Na Mafanikio.

By | July 10, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Unatumiaje yale unayojifunza kupitia falsafa hii mpya ya maisha kufanya maisha yako kuwa bora zaidi kila siku? Hili ni swali muhimu unalopaswa kujiuliza kila siku. Mwanafalsafa Plato amewahi kunukuliwa akisema unexamined life is note woth living, akiwa na maana kwamba maisha ambayo hayachunguzwi, hayana thamani (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Misingi Minne (4) Ya Maisha Ya Wema.

By | July 3, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunashirikishana mambo muhimu kuhusu maisha ili tuweze kuwa na maisha bora yenye furaha na mafanikio makubwa. Tatizo moja ambalo limekuwa linafanya maisha ya wengi kuwa ya hovyo ni kukosa misingi. Tumekuwa kwenye jamii (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Ni Kiasi Gani Cha Fedha Unahitaji Kuwa Nacho Ili Kuwa Na Maisha Bora Na Yenye Furaha?

By | June 19, 2016

Fedha, fedha, fedha, leo imepata nafasi kwenye falsafa yetu mpya kwa sababu ni moja ya vitu vinavyogusa maisha yetu moja kwa moja. Ni moja ya vitu muhimu sana kwenye maisha yetu baada ya hewa tunayovuta. Hii ni kwa sababu kila kitu kinapimwa thamani kwa fedha, chochote tunachotaka, tunaweza kukipata kwa (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Changamoto Za Kuondoka Kwenye Vifungo Vya Maisha Na Kupata Uhuru Wa Maisha.

By | June 12, 2016

Maisha bora, yenye furaha na mafanikio yanaanza na pale mtu anapokuwa huru kwenye maisha. Ndiyo maana kuna watu wengi ambao kwa nje wanaweza kuonekana wamefanikiwa lakini ndani yao wanaona maisha yao bado hayapo kama ambavyo walitaka yawe. Uhuru wa maisha ndiyo unaoleta kila kitu kwenye maisha, lakini pia uhuru huu (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kwa Nini Hisia Bado Zinatushinda Kudhibiti Na Namna Ya Kuzidhibiti.

By | June 5, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye kipengele chetu cha FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunashirikishana mbinu za kujenga falsafa ambayo itatuwezesha kuwa na maisha bora na yenye mafanikio makubwa. kile tunachotaka kinaanzia ndani yetu na tunapokuwa na falsafa imara tunaweza kujenga maisha imara. Leo tunakwenda kuangalia kitu kimoja ambacho (more…)