Category Archives: FALSAFA MPYA YA MAISHA

Hapa unapata makala zinazokuwezesha wewe kujijengea falsafa mpya ya maisha yako. Ni kupitia falsafa yako ya maisha ndio unaweza kuwa na maisha bora yenye furaha na mafanikio.

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Nidhamu Tatu Muhimu Za Kujijengea Ili Kuwa Na Maisha Bora Kila Siku.

By | November 27, 2016

Maisha yetu ni mkusanyiko wa siku tunazokuwepo hapa duniani. Jinsi unavyoishi vizuri kila siku, ndivyo unavyojijengea maisha ya mafanikio. Kama kila siku yako inakwenda hovyo, basi hata maisha yako yote yatakuwa hovyo. Hivyo kabla hata hatujaangalia maisha yako ya miaka 10, 20 mpaka 50 ijayo yatakuwaje kwako, hebu anza kuangalia (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Uliza Kwanza, Ukamilifu Wa Kanuni Ya Dhahabu Ya Maisha Ya Mafanikio.

By | November 13, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni siku nyingine nzuri kwetu wanafalsafa kukutana, kushirikishana yale muhimu ya kujenga falsafa ya maisha yetu ya mafanikio. Kumbuka lengo la falsafa yetu mpya ya maisha, siyo kujua falsafa ili tuwaringishie watu kwamba sisi ni wanafalsafa, badala yake ni kutuwezesha kuwa na maisha bora. Ni (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Jinsi Ya Kutumia KANUNI YA DHAHABU Kupata Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha Yetu.

By | November 6, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni imani yangu kwamba upo vizuri na unaendelea kuweka juhudi kubwa ili kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Kumbuka kwamba falsafa ni sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku, jijengee falsafa imara itakayokusaidia kufanya maamuzi bora ya maisha yako. Ipo kanuni ya Dhahabu (GOLDEN (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Maadui Wakubwa Wawili (02) Wa Furaha Kwenye Maisha Yetu.

By | October 23, 2016

Dhumuni kuu la falsafa kwenye maisha yetu ni kutuwezesha kuwa maisha bora, yenye furaha na mafanikio. Na kama ambavyo tumeshajifunza tena na tena na tena, furaha yetu haitokani na kitu kingine chochote ambacho kipo nje yetu. Furaha yetu inaanzia ndani yetu, furaha hailetwi na vitu au watu, bali tunaitengeneza sisi (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Unawezaje Kuwa Mtu Mzuri?

By | October 16, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri na juhudi zako za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Naamini unaendelea kufanyia kazi falsafa yako ya maisha, ili uweze kuona maana ya maisha yako kwako na kwa wengine pia. Hii ni hatua muhimu sana kwa ukuaji na mafanikio (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kitu Kimoja Kibaya Ambacho Hatuwezi Kukikwepa, Na Jinsi Ya Kuishi Nacho Kwa Furaha.

By | October 9, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni matumaini yangu kwamba uko vizuri na unaendelea kuboresha maisha yako kupitia falsafa ambayo umekuwa unajijengea kila siku. Endelea kuyafanya maisha yako kuwa bora kila siku maana kadiri siku zinakwenda, tunapaswa kuwa bora zaidi. Leo tunakwenda kuangalia jambo moja muhimu sana kwenye maisha yetu, siyo (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Maisha Siyo Mabaya Kama Unavyoaminishwa Kila Siku.

By | October 2, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu kwenye makala yetu ya leo ya falsafa mpya ya maisha, ambapo tunapena maarifa sahihi ya jinsi ya kuishi maisha yetu, kwa ubora na furaha. Unaishi hivyo unavyoishi kutokana na falsafa ya maisha ambayo umeibeba. Tatizo la jamii zetu ni kwamba hatuchagui wenyewe falsafa ya (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Sarafu Ya Maisha Yetu Na Jinsi Tunavyoweza Kuitumia Kufanya Maisha Yetu Kuwa Bora Zaidi.

By | September 11, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena kwenye makala yetu ya leo ya FALSAFA MPYA YA MAISHA, ambapo tunakwenda kushirikishana misingi muhimu ya kuendeshe maisha yetu, ili tuweze kupata kile tunachotaka na kuwa na maisha bora na yenye furaha. Kabla hatujaingia kwenye makala ya leo ya falsafa, naomba nikukumbushe mambo (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; KWA NINI TANO(5), Njia Ya Uhakika Ya Kutatua Tatizo Lolote Ulilonalo.

By | September 4, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Hongera kwa kuendelea kutengeneza falsafa ya maisha yako, ili uweze kuwa na msingi imara wa kufanya maamuzi muhimu ya maisha yako. bila ya kuwa na falsafa, bila ya kuwa na kitu unachosimamia, utakuwa unapelekwa na kila kitu kama bendera inavyopelekwa na upepo. Hayo siyo maisha (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Jinsi Ya Kuondoa Unafiki Kwenye Maisha Yetu, Kipi Unajifanya Huoni?

By | August 28, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena kwenye falsafa yetu mpya ya maisha, ambapo tunakwenda kujifunza njia bora za kuyafanya maisha yetu kuwa bora, yenye furaha na mafanikio makubwa. kama ambavyo nimekuwa nasema kila mara, maisha bila ya falsafa ni maisha ambayo hayana ramani wala mwelekeo, ni maisha ambayo yanaweza (more…)