Category Archives: FALSAFA YA USTOA

Falsafa ya Ustoa (STOICISM) ni falsafa inayotufundisha jinsi ya kuwa na maisha bora na yenye furaha. Ni falsafa inayotfundisha namna ya kuishi maisha yenye maana kwetu na wale wanaotuzunguka. Inatufundisha namna ya kuishi kwa sheria za asili na kuwa na mategemeo sahihi kwenye maisha yetu.
Karibu usome makala za falsafa hii ya Ustoa.

Barua ya IV; Kuhusu hofu ya kifo.

By | May 26, 2023

Barua ya IV; Kuhusu hofu ya kifo. Rafiki yangu Mstoa,Moja ya hofu ambazo zimekuwa zinatusumbua sana sisi binadamu, ni hofu ya kifo.Sote tunajua kuna siku tutakufa, siku ambayo hatuijui. Lakini kila tunapofikiria kuhusu kifo, huwa tunaingiwa na hofu kubwa. Hofu ya kifo imekuwa moja ya vitu vinavyowazuia watu wasiyaishi maisha (more…)

Vitu Vinne Muhimu Ambavyo Mtu Anapaswa Kuvijua Kuhusu Yeye Mwenyewe Ili Aweze Kujitambua Na Kuishi Maisha Halisi Kwake

By | May 20, 2023

Kuishi maisha ya wengine ndiyo chanzo cha wengi kuwa na maisha magumu. Angalia hata maisha yako binafsi, ukiishi kwa mahitaji yako ya msingi na ukiishi maisha yako wala hutajikuta unaumia. Ili tuweze kuishi maisha yetu, falsafa ya ustoa inatusisitiza sana tujitambue sisi wenyewe ili tusisumbuke na mambo yasiyo sahihi kwetu. (more…)

Barua ya III; Urafiki wa kweli na wa uongo.

By | May 19, 2023

Barua ya III; Urafiki wa kweli na wa uongo. Rafiki yangu Mstoa,Kuna watu ambao huwa tunawachagua wawe karibu yetu kwenye maisha.Watu hao, hatulazimiki kuwa nao kama ilivyo kwa ndugu, bali tunakuwa tumechagua kwa hiari yetu wenyewe kuwa karibu nao.Watu hao ni marafiki. Marafiki ni watu muhimu sana kwenye maisha yetu.Ni (more…)

Jinsi Ya Kujiandaa Na Magumu

By | May 6, 2023

Rafiki yangu mstoa, wiki iliyopita tulijifunza jinsi ya kukabiliana na magumu na tuliona kwamba magumu ni sehemu ya maisha. Na magumu hayo huwa yanatuumiza sana pale hatuyategemei kwani huwa yanatokea kwa mshtukizo kama vile ajali, kitu ambacho huwa kinatuumiza sana. Ili kuondokana na hali hiyo, wastoa walikuwa wanajiandaa na zoezi (more…)

Barua ya I; Tumia muda wako vizuri.

By | May 5, 2023

Barua ya I; Tumia muda wako vizuri. Rafiki yangu Mstoa, Muda ni rasilimali muhimu sana kwenye maisha yetu.Ndiyo rasilimali pekee ambayo ukiipoteza huwezi kuipata tena.Lakini pamoja na upekee huo wa muda, bado watu wengi hawana udhibiti na muda wao, hivyo kuishia kuupoteza. Unaweza kudhani changamoto ya muda ni kwa zama (more…)

Jinsi Ya Kukabiliana Na Magumu

By | April 29, 2023

Kila mmoja wetu kuna magumu fulani ambayo anapitia kwenye maisha yake. Na kwa binadamu ni kitu cha kawaida kabisa lakini sisi binadamu pale mambo yanapokuwa shwari tunasahau kama kuna magumu ambayo tunaweza kukutana nayo. Kwa mfano, kama kwa sasa unafurahia jua na kinyume chake kinakuhusu. Falsafa ya Ustoa inatufundisha kuwa (more…)

Mazoezi 10 Ya Falsafa Ya Ustoa Yatakayofanya Uwe Na Maisha Bora.

By | April 28, 2023

Mazoezi 10 Ya Falsafa Ya Ustoa Yatakayofanya Uwe Na Maisha Bora. Habari Mstoa Mwenzangu,Karibu kwenye mwendelezo wa mafunzo yetu ya falsafa ya Ustoa, mafunzo ambayo ni ya kutuwezesha kuchukua hatua ili kuwa na maisha bora. Hapa tunakwenda kujifunza mazoezi kumi ya Falsafa ya Ustoa, ambayo tukiyafanya kuwa sehemu ya maisha (more…)

Jinsi Ya Kukabiliana Na Hasira

By | April 22, 2023

Hasira ni miongoni mwa hisia hasi ambayo imekuwa ikiwagharimu watu wengi. Mpaka sasa hakuna mtu ambaye anaweza kusema hajawahi kufanya maamuzi ya hasira ambayo yalipelekea kuharibu kazi, biashara na hata kuvunja mahusiano yetu. Tatizo la hasira ni ukichaa wa muda na Mwanafalsafa Seneca anafananisha hasira na ukichaa wa muda. Kwa (more…)

Misingi Mikuu Kumi Ya Falsafa Ya Ustoa.

By | April 21, 2023

Misingi Mikuu Kumi Ya Falsafa Ya Ustoa. Ustoa ni falsafa ya vitendo iliyoanzia Ugiriki ya kale na baadaye kuhamia Roma ya kale.Falsafa hii ilianzishwa na Zeno ambaye alikuwa mfanyabiashara na kwenye moja ya safari zake za kibiashara meli yake iliharibika na kupata hasara kubwa. Ni katika kutafuta namna ya kujiliwaza (more…)