Category Archives: FALSAFA YA USTOA

Falsafa ya Ustoa (STOICISM) ni falsafa inayotufundisha jinsi ya kuwa na maisha bora na yenye furaha. Ni falsafa inayotfundisha namna ya kuishi maisha yenye maana kwetu na wale wanaotuzunguka. Inatufundisha namna ya kuishi kwa sheria za asili na kuwa na mategemeo sahihi kwenye maisha yetu.
Karibu usome makala za falsafa hii ya Ustoa.

HUZUNI – Jinsi ya kushinda machozi kwa fikra.

By | April 9, 2017

  Pale tunapopata misiba, hasa ya watu wa karibu kwetu, kama watoto, wazazi na hata ndugu, tunapitia kipindi cha huzuni. Lakini vipi kwa falsafa ya ustoa? Kwa sababu huzuni ni hisia hasi na wastoa hawakubali kutawaliwa na hisia hasi. Seneca anatuambia ya kwamba, ni wajibu wetu kuhuzunika, maana hatuwezi kuzuia (more…)

MATUSI ; Jinsi ya kukabiliana na dharau za wengine.

By | April 9, 2017

Lengo kuu la ustoa ni kuwa na maisha yenye utulivu, kuwa na hisia chanya na kutokukubali yeyote avuruge utulivu wetu na hisia zetu. Lakini tunazungukwa na watu ambao maneno yao na hata vitendo vyao vinaweza kuwa dhihaka au matusi kwetu. Tunapotukanwa au kudharauliwa na wengine, tunapata hasira na hasira hizo (more…)

MAHUSIANO YA KIJAMII – Namna ya kwenda na wengine.

By | April 9, 2017

Dhumuni kuu la wastoa ni kuwa na maisha yenye utulivu. Lakini utulivu huu unaweza kuvurugwa na wengine. Hasa pale tunapohitaji kufanya kazi pamoja na wengine ambao tabia zao siyo sawa na zetu. Hivyo wastoa wanashauri mtu uchague tabia muhimu kwako na kuendesha maisha yako kwa tabia hizo. Na kwa yeyote (more…)

Ushauri wa kistoa – JUKUMU LA KUPENDA UTU.

By | April 9, 2017

Sisi binadamu hatupo hapa duniani peke yetu, tumezungukwa na wenzetu ambao wanaweza kuwa faida kwetu kwa upendo na urafiki. Pia watu hawa wanaweza kuwa chanzo cha hisia hasi kwetu kama hasira na wivu. Watu wanaweza kufanya mambo ya kutuudhi au kushindwa kufanya mambo na ikapelekea sisi kuumia. Marcus Aurelius anasema, (more…)

Mbinu za kisaikolijia za kistoa – KUTAFAKARI/TAHAJUDI.

By | April 9, 2017

  Mwanafalsafa Seneca anatukumbusha kwamba kila siku tunahitaji kupata muda wa kutafakari kuhusu maisha yetu na kile tulichofanya siku nzima. Mwisho wa siku, tunahitaji kupata muda wa kujiuliza siku yetu imekwendaje na yale tuliyofanya tumefanyaje. Ni yapi ambayo tumefanya vizuri, Yapi ambayo tumekosea na Yapi ambayo tunaweza kuboresha zaidi. Epictetus (more…)

Mbinu za kisaikolijia za kistoa – KUJINYIMA MWENYEWE.

By | April 9, 2017

Moja ya mizigo mikubwa ambayo watu wanajijengea wenyewe ni tamaa na kupenda raha. Hivyo watu wengi hukazana sana kuhakikisha kwamba wanapata kila raha wanayotaka. Lakini mtego unakuja, pale wanapopata raha hiyo, wanakiwa na hofu ya kuipoteza na hivyo wanashindwa kuifurahia raha waliyopata. Wastoa wanatushirikisha mbinu mbili muhimu za kuweza kuondokana (more…)

Fatalism; kuishi kama asili ilivyopanga.

By | April 9, 2017

Watu wengi wa enzi za roma, watu waliamini ya kwamba, hatima ya mtu imeshapangwa. Yaani hata ufanye nini, hakuna namna unavyoweza kubadili hatima ya maisha yako. Na hii ilipelekea wengi kutokuhamasika kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yao. Lakini wastoa walijua namna bora ya kutumia hilo, badala tu ya kukubali na (more…)

Utatu wa udhibiti.

By | April 9, 2017

  Wastoa wanaelewa kwamba hawawezi kudhibiti kila kitu kinachotokea kwenye maisha yao. Na kwa vile mambo mengi yanayotokea yanatuathiri moja kwa moja, yana mchango kwenye furaha yetu kwenye maisha. Hivyo ili kuwa na maisha yenye furaha na yasiyoingiliwa na yale yanayoendelea, wanafalsafa wa ustoa walishauri tuyagawe mambo yanayotokea kwenye makundi (more…)

Mbinu za kisaikolojia za ustoa; kutengeneza taswira hasi.

By | March 18, 2017

  Ni tabia ya binadamu kuwa na hamu na kuthamini kitu sana kabla ya kukipata, lakini akishakipata thamani yake inashuka. Ukichukulia watu wanaoshinda bahati nasibu, siku za kwanza wanakuwa na furaha lakini haidumu, wanarudi kwenye maisha yao ya kawaida. Pia mtu anaweza kusoma miaka mingi, akafaulu, akaomba kazi akiwa na (more…)

Wastoa wa Roma.

By | March 18, 2017

  Wastoa wa roma ndiyo waliochangia sana ukuaji wa falsafa ya ustoa. Japo wapo wanafalsafa wengi wa roma, wanne wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye ukuaji wa falsafs hii. Wa kwanza alikuwa Seneca, huyu ni mstoa aliyetambulika kwa kuandika sana. Ndiye mstoa ambaye maandiko yake mengi yamepona mpaka sasa. Aliandika (more…)