Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3192; Maarifa, Maadili na Ujuzi.

By | September 27, 2023

3192; Maarifa, Maadili na Ujuzi. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye ukurasa uliopita wa 3191 tumejifunza kuhusu Ujuzi, Tabia Na Muda.Kwenye ukurasa huu tunakwenda kupata toleo la watoto la vitu vitatu muhimu kuwajengea ili kuwaandaa kwa maisha ya mafanikio. Lakini kabla ya kuingia kwenye ukurasa huu, nianze kwa kuambiana ukweli sisi kama wazazi.Wengi (more…)

3191; Ujuzi, Tabia Na Muda.

By | September 26, 2023

3191; Ujuzi, Tabia Na Muda. Rafiki yangu mpendwa,Hali ya watu kutafuta njia ya mkato ya kupata mafanikio halijaanza leo na wala halitaisha leo.Tangu enzi na enzi watu wamekuwa wanatafuta hizo njia za mkato.Lakini kwa bahati mbaya sana, wamekuwa wanaishia kupoteza nguvu, fedha na muda.Haijawahi kuwepo njia ya mkato ambayo inampa (more…)

3190; Unachokosea kwenye msimamo.

By | September 25, 2023

3190; Unachokosea kwenye msimamo. Rafiki yangu mpendwa,Moja ya vitu ambavyo tumekuwa tunasisitizana sana kwenye hii safari yetu ya mafanikio makubwa ni msimamo.Ambapo ni kufanya bila ya kuacha, liwake jua au inyeshe mvua.Bila ya kufanya jambo kwa msimamo bila ya kuacha, huwezi kupata mafanikio makubwa. Wapo watu wanasikia hili la msimamo (more…)

3189; Unaanza na kufanya.

By | September 24, 2023

3189; Unaanza na kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Kinachowakwamisha watu wengi kupata kile wanachotaka kwenye maisha yao ni kushindwa kuelewa jinsi mipango, hamasa na ufanyaji vinavyohusiana. Hivyo wengi huwa wanatumia muda wao mwingi kupanga nini watafanya. Na hata baada ya kupanga, bado wanatumia muda mwingi kupitia mipango waliyojiwekea. Halafu wanakuja kusubiri mpaka (more…)

3188; Ni milioni tu.

By | September 23, 2023

3188; Ni milioni tu. Rafiki yangu mpendwa,Mwenzetu hapa, Martin Tindwa, anaandika kitabu ambacho anakiita Jilipe Wewe Mwenyewe. Ni kitabu kuhusu mpango binafsi wa kifedha wa kujilipa wewe mwenyewe kwanza kwenye kila kipato ambacho mtu unaingiza. Kwenye kitabu hicho, Martin kuna dhana moja muhimu sana ambayo ameizungumzia na ina uzito mkubwa (more…)

3187; Siyo ngumu kihivyo.

By | September 22, 2023

3187; Siyo ngumu kihivyo. Rafiki yangu mpendwa,Watu wengi wamekuwa wanalalamika maisha ni magumu na kuna ukweli fulani kwenye hilo.Lakini bado tukiangalia kwenye uhalisia, maisha siyo magumu kihivyo, bali watu wenyewe wamekuwa wanazidisha ugumu wa maisha kwa mambo wanayofanya. Kwa mfano kwa walio wengi, kuamka asubuhi na mapema ili kuianza siku (more…)

3186; Mrejesho wa watu.

By | September 21, 2023

3186; Mrejesho wa watu. Rafiki yangu mpendwa,Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii, huwa tunapenda sana kuwa ndani ya kundi la watu.Ili kujihakikishia nafasi yetu kwenye kundi lolote tulilopo, huwa tunajali sana kuhusu mrejesho wa watu wengine kuhusu sisi. Huwa tunataka sana kukubalika na kila mtu, tukiamini ndiyo njia salama ya (more…)

3185; Mateso unayoyafurahia.

By | September 20, 2023

3185; Mateso unayoyafurahia. Rafiki yangu mpendwa,Huwa kuna kauli inayosema watu waliofanikiwa wanakuwa wamefanya vitu ambavyo wasiofanikiwa hawapendi kuvifanya. Pia ni vitu ambavyo wao wenyewe hawapendi kuvifanya, ila wanakuwa hawana namna bali kuvifanya. Ukweli ni kwamba huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kufanya yale ambayo kila mtu anayafanya, tena kwa namna ambavyo (more…)

3184; Haina Mjadala.

By | September 19, 2023

3184; Haina Mjadala. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye safari ya kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha, lazima uwe na mchakato ambao unaufuata mara zote bila kuacha.Unapaswa kuwa na mambo ambayo utayafanya bila ya kuruhusu hofu au sababu zozote zile kukuzuia.Hii ni dhana inayoitwa Haina Mjadala (Non Negotiable). Kwenye mambo hayo, hupotezi muda kujiuliza (more…)

3183; Nini naweza kupenda kwake?

By | September 18, 2023

3183; Nini naweza kupenda kwake? Rafiki yangu mpendwa,Wateja tulionao kwenye kile tunachouza ni watu muhimu sana kwetu.Hao ndiyo wanaotuwezesha kulipa gharama mbalimbali kwenye maisha yetu. Ni kupitia wao kununua kwetu ndiyo tunapata fedha za kuyaendesha maisha yetu.Wateja wanaonunua kwetu ni watu muhimu sana kwetu. Swali ni je tunawafanyaje ili waweze (more…)