Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3162; Kufanya na kutokufanya.

By | August 28, 2023

3162; Kufanya na kutokufanya. Rafiki yangu mpendwa,Kila mtu huwa anakosea kwenye maisha.Hayupo hata mmoja ambaye anapatia mara zote.Tunachotofautiana ni aina ya makosa, ukubwa na madhara. Hapa tutaangalia aina ya makosa na jinsi yanavyowatofautisha watu kwenye matokeo wanayopata. Kuna aina mbili za makosa.Aina ya kwanza ni makosa ya kufanya. Hapa ni (more…)

3161; Nipe nikupe haitoshi.

By | August 27, 2023

3161; Nipe nikupe haitoshi. Rafiki yangu mpendwa,Sehemu kubwa ya mahusiano yetu sisi binadamu yamejengwa kwenye msingi wa nipe nikupe.Kwa sababu kwa asili watu ni wabinafsi, ambao wanajali zaidi maslahi yao kuliko maslahi ya watu wengine. Kupitia hilo la watu kujali zaidi maslahi yao binafsi, ndiyo kanuni kuu ya ushirikiano na (more…)

3160; Mafiga matatu.

By | August 26, 2023

3160; Mafiga matatu. Rafiki yangu mpendwa,Hendry Ford hakuwa injinia.Wala hakujua kitu chochote kuhusu fizikia.Lakini alikuwa mmiliki wa kampuni ya magari. Siku moja Ford alipata wazo.Kwamba inawezekana injini ya gari ikawa na uwezo mkubwa zaidi. Na hilo litawezekana kama injini itakuwa na pistoni 8 badala ya 6 zilizozoeleka.Aliona hilo ni wazo (more…)

3159; Maokoto.

By | August 25, 2023

3159; Maokoto. Rafiki yangu mpendwa,Fedha ndiyo kitu ambacho huenda kina majina mengi ya utani kuliko kitu kingine chochote.Fikiria majina mbalimbali ya fedha kama mshiko, mapene, ngawira, fuba au shekeli.Yote hayo ni majina ya fedha yamekuwa yakitumika katika nyakati mbalimbali. Na kwa wakati wa sasa, jina maarufu la fedha ni maokoto.Binafsi (more…)

3158; Mateso bila chuki.

By | August 24, 2023

3158; Mateso bila chuki. Rafiki yangu mpendwa,Tumechagua kuingia kwenye hizi biashara tunazofanya kwa sababu mbalimbali. Lakini sababu kubwa kabisa ni kupata uhuru kamili kwenye maisha yetu.Yaani kuanzia kupata uhuru wa kifedha, muda, eneo na watu. Lakini matokeo ambayo watu wengi wanaoingia kwenye biashara wanayapata ni tofauti kabisa na matarajio wanayokuwa (more…)

3157; Akili na Kipaji.

By | August 23, 2023

3157; Akili na Kipaji. Rafiki yangu mpendwa,Hapa nina habari nzuri na mbaya kwako. Na tutaanza na habari mbaya.Habari mbaya ni kwamba ili upate mafanikio makubwa unahitaji kuwa na akili kubwa na kipaji cha kipekee.Na ubaya wa habari hiyo ni kwamba hivyo ni vitu viwili ambavyo huwezi kuvibadili.Huwezi kujiongeza akili wala (more…)

3156; Hakuna ‘ni mara moja tu’.

By | August 22, 2023

3156; Hakuna ‘ni mara moja tu’. Rafiki yangu mpendwa,Huwa tunaweka malengo na mipango mbalimbali ya mambo gani tutafanya na yapi ambayo hatutayafanya.Tunafanya hivyo kwa nia njema kabisa ya kuweza kupiga hatua ambazo tumepanga kupiga. Lakini inapokuja kwenye utekelezaji, mambo ndiyo huwa magumu sana kufanya kama ulivyopanga.Mtu unashawishika kwenda kinyume na (more…)

3155; Uhitaji na Upatikanaji.

By | August 21, 2023

3155; Uhitaji na Upatikanaji. Rafiki yangu mpendwa,Msingi mkuu wa uchumi umejengwa kwenye kanuni ya Uhitaji na Upatikanaji (Demand and Supply).Kanuni hiyo inasema kitu kinapokuwa na uhitaji mkubwa kuliko upatikanaji wake, thamani yake inakuwa kubwa zaidi. Kwa lugha rahisi ni kwamba kama vitu ni vichache na wanaovitaka ni wengi, bei inakuwa (more…)

3154; Tofauti itakapoanzia.

By | August 20, 2023

3154; Tofauti itakapoanzia. Rafiki yangu mpendwa,Siku ya jana, mjasiriamali na mwandishi Alex Hormozi alikuwa na tukio kubwa kabisa la kuzindua kitabu chake cha pili kinachoitwa $100M Leads. Ni kitabu cha kutengeneza wateja tarajiwa kwenye biashara, ambapo ndani yake ameeleza njia nane za uhakika za kutengeneza wateja tarajiwa wengi kwenye biashara (more…)

3153; Kiburi cha umasikini.

By | August 19, 2023

3153; Kiburi cha umasikini. Rafiki yangu mpendwa,Tofauti kati ya matajiri na masikini imekuwa inaendelea kukua kwa kasi kubwa.Masikini wamekuwa wanaendelea kuwa masikini zaidi na zaidi, huku matajiri wakiendelea kupata utajiri mkubwa zaidi na zaidi. Wengi wamekuwa wanatoa sababu zao mbalimbali juu ya tofauti hiyo, lakini zimekuwa ni za juu juu (more…)