Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3143; Kikosi cha kwanza.

By | August 9, 2023

3143; Kikosi cha kwanza. Rafiki yangu mpendwa,Kila kocha wa mchezo, huwa ana wachezaji wengi kuliko inavyohitajika.Kwenye wachezaji hao wengi anaokuwa nao, huwa ana kikosi chake cha kwanza. Kikosi cha kwanza huwa kinakuwa na wale wachezaji bora kabisa ambao kocha anakuwa na imani nao kwamba wanaweza kumpa ushindi mkubwa.Hicho ndiyo kikosi (more…)

3142; Sikosi hela ya kula.

By | August 8, 2023

3142; Sikosi hela ya kula. Rafiki yangu mpendwa,Matokeo yoyote ambayo mtu unayapata yanalingana na fikra ambazo mtu unakuwa nazo.Unachopata ni sawa sawa kabisa na picha uliyonayo kwenye fikra zako. Kwa mfano kama kwenye fikra zako unajisifu kwamba kwenye shughuli zako hukosi hela ya kula, hicho ndiyo utakachoishia kupata, hela ya (more…)

3141; Kwa nini hufanyi?

By | August 7, 2023

3141; Kwa nini hufanyi? Rafiki yangu mpendwa,Unajua unachotaka kwenye maisha yako, wapi unapotaka kufika.Pia unajua nini unapaswa kufanya ili uweze kupata unachotaka.Lakini sasa, kwa nini hufanyi yale unayopaswa kufanya ili kupata unachotaka kupata? Na hata pale inapotokea unaanza kufanya, kwa nini huna mwendelezo?Kwa nini unaanza kufanya na kuishia njiani?Nini kinakukosesha (more…)

3140; Chukua picha nyingi zaidi.

By | August 6, 2023

3140; Chukua picha nyingi zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Siku moja ya tarehe 10 Disemba mwaka 1914, Thomas Edison akiwa nyumbani kwake alipata taarifa kwamba maabara yake kubwa ilikuwa inaungua moto.Aliongozana na kijana wake kwenda kuangalia hilo na kukuta kweli maabara ikiteketea kwa moto.Baada ya kuona kinachoendelea, Edison aligeuka na kumwambia kijana (more…)

3139; Dola.

By | August 5, 2023

3139; Dola. Rafiki yangu mpendwa,Kwa zama tunazoishi sasa, sifa za utajiri huwa zinapimwa kwa thamani ya dola za Kimarekani.Huenda hilo likaja kubadilika kwa zama zijazo, ila kwa sasa hicho ndiyo kipimo. Hivyo basi, inapokuja kwenye kiwango cha utajiri ambacho mtu amefikia, thamani inayotumika ni ya dola.Na kinachopimwa ni thamani ya (more…)

3138; Malengo potoshi.

By | August 4, 2023

3138; Malengo potoshi. Rafiki yangu mpendwa,Kila mtu kwenye maisha ana malengo. Wanaofanikiwa wanakuwa na malengo.Kadhalika pia kwa wale wanaoshindwa, huwa wanakuwa na malengo pia. Hapa unaweza kujiuliza tofauti ya watu inatokea wapi kama wote wana malengo?Jibu ni kwamba tofauti inaanzia kwenye ubora wa malengo.Watu wanaofanikiwa huwa wanakaa chini na kuweka (more…)

3137; Hivi kesho jua litachomoza?

By | August 3, 2023

3137; Hivi kesho jua litachomoza? Rafiki yangu mpendwa,Hebu fikiria kama hilo ndiyo swali ambalo ungekuwa unajiuliza kila siku kabla ya kulala, iwapo jua litachomoza au la.Fikiria ingebidi ujiulize hivyo kwa sababu jua linakuwa halieleweki, kuna siku linachomoza na kuna siku halichomozi kabisa au linachelewa.Unadhani maisha yako yangekuwa sawa na yalivyo (more…)

3136; Ukatili wa asili.

By | August 2, 2023

3136; Ukatili wa asili. Rafiki yangu mpendwa,Asili huwa inafanya maamuzi yake kwa namna yake yenyewe.Maamuzi yanayofanywa na asili huwa hayaangalii matakwa ya watu. Kama asili ingekuwa ni mtu kwenye hayo maeneo yote yanayofanyiwa maamuzi, angeonekana kuwa mtu mwenye roho mbaya sana na asiyejali.Hiyo ni kwa sababu watu watakuwa na maelezo (more…)

3135; Utamchagua nani?

By | August 1, 2023

3135; Utamchagua nani? Rafiki yangu mpendwa,Safari yetu ya mafanikio makubwa tunayoyataka inawategemea sana watu.Hakuna namna tunaweza kufikia mafanikio makubwa kabisa sisi peke yetu. Kadiri lengo letu la mafanikio linavyokuwa kubwa, ndivyo pia idadi ya watu tunaowahitaji inavyokuwa kubwa zaidi.Hivyo sehemu kubwa sana ya maamuzi utakayokuwa unayafanya kila siku ni kuhusu (more…)

3134; Maswali mawili yatakayokuwezesha kuuza zaidi.

By | July 31, 2023

3134; Maswali mawili yatakayokuwezesha kuuza zaidi. Rafiki yangu mpendwa,Leo napenda nikupe taarifa ambazo zitakushtua kidogo.Taarifa hizo zitakushtua kwa sababu ni tofauti kabisa na matarajio uliyonayo. Kwenye biashara yako una wateja ambao tayari wananunua kwako mara kwa mara.Lakini je unajua ni kwa kiasi gani wateja hao wanajua vitu vyote unavyoweza kuwauzia? (more…)