Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

3114; Viwango na mipaka.

By | July 11, 2023

3114; Viwango na mipaka. Rafiki yangu mpendwa,Maisha huwa ni magumu, lakini huwa tunayafanya kuwa magumu zaidi kwa kutaka kudhibiti mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu. Moja ya vitu ambavyo huwa tunapenda sana kufanya ni kuwabadili watu.Watu mbalimbali ambao tunachagua kushirikiana nao kwenye maeneo mbalimbali, wanakuwa na tabia ambazo ni (more…)

3113; Una kitu, utafika mbali.

By | July 10, 2023

3113; Una kitu, utafika mbali. Rafiki yangu mpendwa,Leo nataka nikupe maua yako, nikupe sifa kwa vitu ulivyonavyo, ambavyo ukiamua kuvitumia vizuri, utafanya makubwa sana kwenye maisha yako.Ni vitu ambavyo unaweza kuwa unavichukulia kawaida, lakini kama utavipa uzito, utaweza kufikia malengo makubwa uliyonayo. Wewe kuwa hai mpaka sasa ni kitu kikubwa (more…)

3112; Anzia mahali.

By | July 9, 2023

3112; Anzia mahali. Rafiki yangu mpendwa,Kama utasubiri mpaka taa zote za barabarani ziwake kijani ndiyo utoke, kamwe hutatoka nyumbani.Unachopaswa kufanya ni kutoka kisha kufuata taa moja moja kadiri inavyoelekeza, iliyo kijani unapita, nyekundu unasubiri iwake kijani.Lakini hapo unakuwa kwenye mwendo na hivyo inakuwa rahisi kuendelea kuliko ukiwa hujaanza kabisa. Kwa (more…)

3111; Kazi yako kuu.

By | July 8, 2023

3111; Kazi yako kuu. Rafiki yangu mpendwa,Mimi siyo Mkatoliki na wala sifungamani na dini yoyote, lakini kuna ujumbe nimekutana nao mtandaoni kuhusu Wakatoliki na nimeona kuna mengi sana ya kujifunza kwenye hii safari yetu ya mafanikio makubwa. Ujumbe huo, unaeleza kama ifuatavyo; “Ninapenda sana kiwango cha Wakatoliki cha kutokusumbuka. Utakosoa (more…)

3110; Raha kufanya.

By | July 7, 2023

3110; Raha kufanya. Rafiki yangu mpendwa,Huwa kuna kauli mbili ambazo huwa zinawachanganya watu wengi.Ya kwanza inasema; Fanya kile unachopenda kufanya na fedha zitakufuata zenyewe.Ya pili inasema; Kama unataka mafanikio makubwa usifanye kazi, bali fanya kile unachopenda. Mkanganyiko ambao umekuwa unatokana na kauli hizo ni imani ambayo watu wengi wanayo kwamba (more…)

3109; Tarehe ya mwisho wa matumizi.

By | July 6, 2023

3109; Tarehe ya mwisho wa matumizi. Rafiki yangu mpendwa,Kila kitu huwa kina tarehe ya mwisho wa matumizi yake (expire date).Hiyo ni tarehe ambayo baada ya hapo kitu hicho hakiwezi kutumika tena. Inaanza na maisha yetu wenyewe, huwa yanaanza pale tunapozaliwa na kuisha matumizi pale tunapokufa.Kila mtu anayo tarehe ya mwisho (more…)

3108; Kuepuka ushindani.

By | July 5, 2023

3108; Kuepuka ushindani. Rafiki yangu mpendwa,Ushindani ni moja ya vikwazo vinavyowazuia watu wengi kupiga hatua kwenye maisha yao.Ushindani mkali unawazuia watu wasipige hatua kubwa. Pamoja na changamoto kubwa ya ushindani, bado ni kitu cha mtu kujitakia.Yaani kama mtu anakabiliwa na ushindani, anakuwa amechagua yeye mwenyewe. Huwa wanasema hakuna foleni kwenye (more…)

3107; Kitu pekee kinachokuzuia.

By | July 4, 2023

3107; Kitu pekee kinachokuzuia. Rafiki yangu mpendwa,Ni ukweli usiopingika kwamba ili kupata mafanikio makubwa, lazima uchukue hatua kubwa sana.Hatua ambazo hujawahi kuzichukua na wala hazijazoeleka kwa wale wanaokuzunguka. Wale wote waliofanikiwa sana, huwa wanalijua hilo vizuri na wanalitekeleza. Wanajua hakuna mbadala wa kuchukua hatua kubwa, hivyo wanaanza kufanya hivyo mapema (more…)

3106; Kitu cha kwanza kufanya kila unapoamka asubuhi.

By | July 3, 2023

3106; Kitu cha kwanza kufanya kila unapoamka asubuhi. Rafiki yangu mpendwa,Kwenye zama tunazoishi sasa, zama za teknolojia ambapo simu zetu janja (smartphones) zimeshika sehemu kubwa ya maisha yetu, huwa ndiyo kitu ambacho tunakigusa mara nyingi zaidi. Huwa natania kwamba mtu anaweza kuamka asubuhi, kabla hata hajajua kama anaweza kutembea au (more…)

3105; Anasa za watu wa kawaida.

By | July 2, 2023

3105; Anasa za watu wa kawaida. Rafiki yangu mpendwa,Watu wa kawaida, ambao ndiyo wengi, huwa hawapati mafanikio makubwa kwenye maisha yao.Na sababu kubwa kabisa inayozuia watu hao wa kawaida wasipate mafanikio ni kusumbuliwa na anasa nyingi ambazo zinahamisha sana umakini wao. Watu hao huwa wanaridhika sana haraka na vitu ambavyo (more…)